Tuesday, April 30, 2013

MSHTUKO!


Na Waandishi Wetu

MAGHOROFA yaliyojengwa kandokando ya Mto Mlalakua na Ufukweni mwa Bahari ya Hindi yatabomolewa, hivyo kuzua mshtuko mkubwa kwa wamiliki.
Uchunguzi  uliofanywa na gazeti hili kwa zaidi ya wiki nne umebaini kwamba kazi ya kubomoa nyumba hizo inaweza kuanza wakati wowote ingawa kuna changamoto kubwa kwani baadhi ya nyumba hizo ni za vigogo wenye madaraka makubwa serikalini au ndani ya vyama vya siasa.

Habari zaidi zinadai kwamba baadhi ya vigogo hao wamekimbilia mahakamani kufungua  kesi ya kupinga nyumba zao zisiguswe wakati wengine wamekua wakitoa vitisho kwa waliopewa…
Na Waandishi Wetu
MAGHOROFA yaliyojengwa kandokando ya Mto Mlalakua na Ufukweni mwa Bahari ya Hindi yatabomolewa, hivyo kuzua mshtuko mkubwa kwa wamiliki.
Uchunguzi  uliofanywa na gazeti hili kwa zaidi ya wiki nne umebaini kwamba kazi ya kubomoa nyumba hizo inaweza kuanza wakati wowote ingawa kuna changamoto kubwa kwani baadhi ya nyumba hizo ni za vigogo wenye madaraka makubwa serikalini au ndani ya vyama vya siasa.
Habari zaidi zinadai kwamba baadhi ya vigogo hao wamekimbilia mahakamani kufungua  kesi ya kupinga nyumba zao zisiguswe wakati wengine wamekua wakitoa vitisho kwa waliopewa mamlaka ya kuzibomoa.
Vyanzo vyetu vya habari vinadai kwamba baadhi ya nyumba hizo zina hati zilizopatikana serikalini wakati zingine wamiliki wao walivamia maeneo hayo na kuporomosha maghorofa makubwa.
Kutokana na ujenzi huo holela, wakazi wa Kawe kwa Malecela waliamua kumwandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Profesa Anna Tibaijuka wakitoa malalamiko juu ya ujenzi huo.
 Barua hiyo ambayo gazeti hili lina nakala yake iliyoandikwa Februari 20, mwaka huu ilieleza kwamba ujenzi wa nyumba hizo umekuwa ni kero kubwa kwani zimejengwa katika mkondo wa maji hivyo mvua inaponyesha inasababisha mafuriko kwa wananchi wengine.
Wananchi hao wamemueleza waziri kwamba nyumba hizo zimeziba mkondo wa maji katika baadhi ya mito inayoingia baharini, hivyo kusababisha maji kuhama na kuelekea kwenye nyumba zao na daraja la eneo la Malecela kusombwa na maji hivyo kusababisha magari kutopita.
Walidai kuwa nyumba nyingi zimejengwa katikati ya mto na wengine wamejaza vifusi kando ya mto unaopita karibu na nyumba zao, hivyo kusababisha mkondo wa maji kwenda kwa wananchi.
“Hivi sasa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanashindwa  kutembelea ufukwe wa bahari kutokana na baadhi ya nyumba kuziba njia na mbaya zaidi waliojenga kando ya mkondo wameharibu mikoko,” imesema sehemu ya barua hiyo.
Waliendelea  kusema kwamba vigogo hao  ambao ni wavamizi baadhi yao wamekuwa wakitembea na bastola hadharani na   kuwatishia maisha wale wanaodiriki kuzungumzia ujenzi wanaoufanya katika maeneo hayo.
Wananchi hao wametishia kuwa endapo hawatasikilizwa wataenda Ikulu kumuona Rais Jakaya Kikwete.
Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Hifadhi ya Mazingira nchini (NEMC),  Ignas Mchallo alisema:
“Wote waliojenga katika maeneo hayo  watahamishwa kwa kufuata sheria kwani kuna wengine waliojenga kabla ya sheria ya mazingira ambayo inataka kuwepo kwa nafasi ya mita 60 toka mtoni au ufukweli,” alisema Mchallo.
Tahadhali iliyopo eneo la majengo hayo.
Naye  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema  kwamba nyumba 73 zilizojengwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi, zitavunjwa na akazitaja kuwa ziko kwenye fukwe za Kawe, Mbezi na Msasani na kwamba ingawa zilijengwa kihalali baada ya kupewa hati, lakini sheria mpya hairuhusu nyumba hizo kuwepo.

"KUNA MAJAMBAZI WAMETUMWA NA VIGOGO WAJE KUNIUA".......MAMA ZITTO...!!

SHIDA Salum ambaye ni mama mzazi wa mwanasiasa machachari ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema kuna watu wanataka kumuua. 



Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita, Shida alisema Aprili 19, mwaka huu, saa moja na nusu katika Ghorofa la NSSF maeneo ya Tabata Bima, hawezi kuisahau kwa kuwa ndiyo siku ambayo majambazi walimvamia wakiwa na bastola.
Akisimulia mkasa huo Shida alikuwa na haya ya kusema:
“Majambazi hayo yaliyonivamia siyajui lakini mmoja wao huwa namuona. Kabla hawajaja walinipigia simu wakaniambia wana shida na mimi lakini hatukupanga namna ya kuonana.
Uwazi: Sasa walipofika nyumbani kwako, uliwakaribishaje?
Shida: Walipofika walivamia na kufanikiwa kuingia sebuleni.
Uwazi: Baada ya kuingia ikawaje?
Shida: Cha kwanza walichotaka ni laptop (Kompyuta mpakato), flash na simu zangu.
Uwazi: Uliwapa?
Shida: Baada ya kutoa amri hiyo niliwajibu kuwa kompyuta iko ofisini na simu niliwaambia ziko kwenye chaji.
Uwazi: Baada ya hapo ikawaje?
Shida: Mmoja wa majambazi hayo alinionyesha bastola kuwa kama sijatii hayo wanayoniambia basi watanifanya kitu kibaya,   ndipo nikamuita kijana wangu aitwaye Mtana aende chumbani kuchukua simu zangu niwape.
Uwazi: Ikawaje?
Shida: Niligundua kuwa Mtana alikuwa anasikia amri zilizokuwa zikitolewa na majambazi hayo, hivyo alipiga kelele kuomba msaada kwa wananchi.
Uwazi: Majambazi wakafanya nini?
Shida: Waliposikia kelele walikimbilia nje, wakaingia ndani ya gari lao ambalo namba zake zisijui, wakatoweka.
Uwazi: Pole sana.
Shida: Pamoja na purukushani hizo namshukuru Mungu sana kwa kuwa hawakunidhuru na hawakufanikiwa kuchukua chochote.
Uwazi lilitinga nyumbani kwa mama huyo na kukuta ulinzi ukiwa umeimarishwa ambapo sasa kuna askari wenye bunduki.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, majambazi hayo yalifanikiwa kuingia ndani baada ya mlinzi aliyekuwepo zamu kwenda kubadili nguo za kiraia ili avae za kiaskari.
“Tukio lilikuwa la haraka sana, wakati askari huyo anatoka kwenye kibanda cha kubadilishia nguo ndipo na wale majambazi walipokuwa wakitoka ndani na kuingia kwenye gari lao,” kilisema chanzo.
Waandishi wetu walimtafuta kiongozi wa walinzi wanaolinda nyumbani kwa mama huyo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Ngosha na alipoulizwa kuhusu sakata la kuvamiwa alikiri kulifahamu.
“Baada ya tukio lile tumeimarisha ulinzi ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao. Sasa tumeweka askari wenye bunduki na tunaamini tukio kama hilo halitajirudia,” alisema Ngosha.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minagi alikiri kutokea kwa tukio hilo.
“Nina taarifa ya tukio hilo na tunaendelea na upelelezi kuwasaka majambazi hao, wananchi waondoe hofu.” alisema Kamanda Minagi.

DOKTA CHENI APATA MTOTO


Msanii wa filamu wa bongo Mahsein Awadh amepata mtoto wa kike hivi karibuni hali iliyosababisha msanii wa maigizo ambaye yupo karibu na msanii huyo Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu kumtakia maisha marefu yenye mafanikio mtoto huyo kupitia mtandao wa Instagram

Msanii Hammer Q amdunda mkewe, Salha, kama mwizi ..Angalia PICHA


Baadhi ya picha za mkewe baada ya kipigooooo.







Nguo za Hammer Q zikiwa zimetapakaa damu hatariiiii.


Kwa mujibu wa zeddylicious Salha alipewa kichapo hiki baada ya kumtambulisha rafiki yake wa kiume ambae ni Tx Moshi kwa mumewe Hammer Q. Inavyosemekana alimpiga mateke, mangumi, akampasulia kioo kichwani, kampiga na jiko la mkaa kichwani n.k 

ALICHOANDIKA MKUU WA WILAYA YA KOLOGWE FACEBOOK KUHUSU WABUNGE WA CHADEMA.


RAISI WA ALGERIA HOI

Abdelaziz-Bouteflika

Afya ya Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, imekua mbaya hadi kusafirishwa Paris nchini ufaransa kwa ajili ya kupata matibabu ya ugonjwa wa kiarusi.
Taarifa rasmi zinaeleza kuwa Jumamosi alipata ugonjwa wa kiarusi kidogo lakini haifikiriwa afya yake itaathirika kwa muda mrefu.
Hata hivyoimeripotiwa na Waziri Mkuu wa Algeria kuwa hali ya Rais huyo siyo mbaya kwasasa. Taarifa rasmi ilieleza kwamba alikuwa na kidonda cha tumbo lakini nyaraka za siri za wana

    JOSE CHAMILION AWAPIGIA DEBE RADIO & WISLE

    Chameleone

    Baada ya kufunika vilivyo kwa kutoa burudani ya nguvu katika tamasha kubwa ambalo limefika huko nchini Uganda hivi karibuni msanii Jose Chameleone amesema kuwa amewaomba mashabiki na wadau kuwapa sapoti wasanii wa Goodlyfe, Moses Radio na Weasel TV.
    Chameleone ambaye ni ndugu na Weasel TV alitumia nafasi hiyo ya kuwaomba mashabiki katika tamasha hilo kutokana na kwamba wasanii hao wamekuwa ni wenye mafanikio makubwa na kwamba katika wiki mbili zijazo wanatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yao waliyoibatiza jina ‘Obudde’.
    Aidha Jose Chameleone alionyesha kuwa yeye ni gwiji na mwenye kipaji katika tamasha lake la ‘Badilisha’ haswa alipoweza kuimba zaidi ya nyimbo 40 ambapo pia aliziimba nyimbo za wasanii mbalimbali Afrika Mashariki kama wimbo wa Kigeugeu wa Jaguar, Mukama wa Judith Babirye, Bread and Butter kutoka kwao Moses Radio na Weasel TV, Kasepiki wa Bebe Cool na Wendi wa Bobi Wine.

      MAGAZETI YA LEO APRILI 30, 2013


      .

      .
      .
      .

      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .
      .

      DADA WA NDIKUMANA APALILIA NDOA YA KAKA YAKE

       
      Uwoya akiwa na mumewe Ndikumana enzi hizo.
      Dada wa mchezaji wa Timu ya Rayon Sport, Ndikumana Katauti, Fatuma amefunguka kuwa licha ya migongano ya ndoa ya kaka yake lakini bado wanapendana. 
      Akizungumza na gazeti moja la nchini Rwanda, Fatuma alisema kwamba hata ilivyotoka habari kuwa wifi yake Irene Uwoya amenaswa na Diamond alishtuka sana kwani yeye bado anaamini ndoa ya kaka yake ina uhai wa asilimia mia moja.

      “Nilishangaa sana kuona gazeti limeandika kuwa wifi yangu amenaswa na Diamond, mimi naamini ndoa ya kaka yangu bado ipo hai,” alisema Fatuma.