Waombolezaji katika msiba nchini Zimbabwe walipigwa na butwaa pale
mtu aliyekufa alipoamka wakati wakipita kando ya jeneza lake kutoa
heshima za mwisho, shirika la habari za nchi hiyo limeripoti jana.
Brighton Dama Zanthe, mwenye miaka 34, aliingizwa ndani ya jeneza
Jumatatu baada ya kuwa amefariki nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda
mrefu.
Familia iliyojawa na huzuni ya mfanyakazi huyo wa usafirishaji
ilifunika mwili wake kwa mablanketi na kufanya mipango ya kumhamishia
kwenye mochari ya mjini humo, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa
katika gazeti la The Herald.
Lakini siku iliyofuata marafiki wa Zanthe na jamaa zake
walisambaratika wakiwa hawaamini pale alipoanza kutembea wakati wakipita
mbele ya jeneza kuaga mwili wa ‘marehemu’ huyo.
Bosi wa ‘marehemu’ huyo, Lot Gaka alieleza kuhusu mkasa huo
alipobaini mfanyakazi wake alikuwa bado angali hai.
Alisema: “Kwanza niligundua miguu ya Zanthe ikisogea wakati
nilipokuwa kwenye ya foleni kutazama mwili wake. Hili lilinishitua mno.
Kwanza sikuweza kuamini macho yangu lakini baadaye nilibaini kwamba
kulikuwa na kusogea kwa viungo kadhaa katika mwili wake huku
waombolezaji wengine wakiwa hawaamini kinachoendelea.”
Gaka, ambaye anaendesha kampuni ya mabasi katika mji wa Gweru,
alisema Zanthe alikuwa hana afya njema kabla ya ‘kifo’ chake wiki
iliyopita.
Alielezea minsi alivyotembelea nyumbani kwa familia hiyo kutoa
msaada pale mke wa mfanyakazi wake alivyompigia simu kumweleza kwamba
Zanthe alikuwa amefariki.
Alisema: “Zanthe alikuwa katika likizo ya ugonjwa kwa kipindi fulani na kila mmoja kazini alikuwa akifahamu kwamba hali yake ilikuwa mbaya.
Alisema: “Zanthe alikuwa katika likizo ya ugonjwa kwa kipindi fulani na kila mmoja kazini alikuwa akifahamu kwamba hali yake ilikuwa mbaya.
“Tulimtembelea nyumbani kwake.
“Sikushangaa pale nilipopokea simu kutoka kwa mke wa Zanthe Jumatatu usiku wiki iliyopita akisema kwamba mume wake alikuwa amefariki.”
“Sikushangaa pale nilipopokea simu kutoka kwa mke wa Zanthe Jumatatu usiku wiki iliyopita akisema kwamba mume wake alikuwa amefariki.”
Aliongeza: “Nilitembelea maduka mawili yanayouza majeneza mjini
humo kwa ajili ya kuulizia gharama kabla ya kuelekea nyumbani kwa Zanthe
hivyo kuweza kuchukua mwili wake na kuuhifadhi katika mochari.
“Mwili wa Zanthe tayari ulishawekwa kwenye jeneza na watu walikuwa
wakijiandaa kwa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho hivyo mwili wake
kuweza kupelekwa mochari.
“Ilikuwa katika wakati huo wa utaratibu wa kutoa heshima ndipo ‘akazinduka’.”
“Ilikuwa katika wakati huo wa utaratibu wa kutoa heshima ndipo ‘akazinduka’.”
Shuhuda mwingine alieleza jinsi familia hiyo ilipovuta mablanketi
hayo kutoka kwenye mwili wa Zanthe huku wakiwa wamechanganyikiwa
kujaribu kumnusuru baada ya kubaini alikuwa bado mzima.
Alisema: “Gaka baadaye aliondoa baadhi ya mablanketi kutoka kwenye
mwili wa Zanthe baada ya kubaini akijitikisa na hii ilikuwa pale wote
tulipobaini kwamba bado kulikuwa na uhai.
“Kisha tuliita gari la wagonjwa ambalo lilikuja katika muda wa ndani ya dakika saba.
“Kisha tuliita gari la wagonjwa ambalo lilikuja katika muda wa ndani ya dakika saba.
“Hakika ni muujiza na wengi wa watu hawaamini.”
The Herald, ambalo linamilikiwa na serikali ya Zimbabwe, liliripoti kwamba Zanthe alikaa siku mbili kwenye mashine ya kusaidia kupumua baada ya kuwa amepelekwa katika Hospitali ya Jimbo la Gweru kufuatia tukio hilo.

Aliruhusiwa wiki iliyopita na kurejea nyumbani kwake.
Familia ya mtu huyo iliyotikiswa ailieleza ana kumbukumbu chache tu ya matukio hayo.
Alisema: “Hii ishu inaweza kusimuliwa vizuri na watu waliofika nyumbani kuhudhuria msiba wangu.
Familia ya mtu huyo iliyotikiswa ailieleza ana kumbukumbu chache tu ya matukio hayo.
Alisema: “Hii ishu inaweza kusimuliwa vizuri na watu waliofika nyumbani kuhudhuria msiba wangu.
“Sifahamu kilichotokea na ninakumbuka tu kuwapo hospitalini kwenye
mashine za kusaidia kupumua.”
Aliongeza: “Kila kitu ni historia kwangu.
“Ninachoweza kuthibitisha ni kwamba watu walikusanyika nyumbani kwangu kuombolezwa lakini nilipatiwa nafasi nyingine na niko hai. Najisikia vizuri sasa.”
Aliongeza: “Kila kitu ni historia kwangu.
“Ninachoweza kuthibitisha ni kwamba watu walikusanyika nyumbani kwangu kuombolezwa lakini nilipatiwa nafasi nyingine na niko hai. Najisikia vizuri sasa.”
No comments:
Post a Comment