Friday, May 24, 2013

KIONGOZI WA VURUGU ZA MTWARA AKAMATWA......!!

vujo mtwara

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                           S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                        DAR ES SALAAM.
24 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi Nchini linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya simu ya mkononi akituma SMS kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na kutoa matusi kwa viongozi hao.


Mtu huyo amekuwa akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia Chips (sim card) 13 za simu za mkononi ambazo amekamatwa nazo. Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtu huyo na ushahidi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
 Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zingine za wahahlifu kama hao kujitokeza na kutoa taarifa hizo polisi ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki, wakiwemo watu wanaowashawishi wenzao kwa njia ya fedha, kuwashauri ama kuwasaidia kwa namna yeyote ile katika kufanikisha uhalifu huo na kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini.
Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.

Wednesday, May 22, 2013

HUYU NDIYE MKENYA ALIYECHINJA WATU 400 KWA PANGA APEWA HIFADHI UINGEREZA.


John Thuo.
Muuaji ambaye aliua karibu watu 400 nchini mwake amepatiwa hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza.

John Thuo, mwenye umri wa miaka 27, ambaye aliwacharanga wengi wa waathirika wake katika mashambulio ya kutumia mapanga nchini kwake Kenya, ametumia takribani miaka 10 akiishi nchini Uingereza kwenye makazi ya bure iliyotolewa na Huduma ya Taifa Kusaidia Hifadhi ya Kisiasa.
Anaaminika kupokea marupurupu yanayofikia Pauni za Uingereza 160 kwa mwezi kutoka huduma hiyo, kitengo cha Wizara ya Mambo ya Ndani kinachoshughulikia makazi kwa wanaotaka hifadhi ya kisiasa.
Thuo, ambaye alikuwa mfuasi wa kundi halifu la Mungiki nchini Kenya, alikiri mbele ya mahakama ya uhamiaji kwamba aliwaua 'takribani watu 100 hadi 400'.

MWANA FA AWAJIA JUU WASANII WAKONGWE KWA TABIA MBAYA YA KUPENDA KULALAMIKA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFng5R5CleiOhOlIxaQq2U-cl-VywkQMTCjQZnirBfmq6z8kn6O2bxrIYZ-KA292-EvIFWTfkbil0Of9ZkJSCWC88Vbrpq3FrwbKv97Q6m_UmZQIGxo3CqSztzyFgn-Qjq9Re6AOM2d7S2/s1600/IMG_09102.jpg

Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema mara nyingi wasanii wakongwe huishia kulalamika wanapochuja kwakuwa hushindwa kubadilika kuendana na wakati na pia kupenda kuchukuliwa kama ‘malegendary’ hata kama wakichemka kwenye kazi zao mpya.Ameongeza kuwa mara nyingi wasanii wengi hufika hatua ya kuanza kulalamika kwakuwa muziki wa Tanzania hauna mipango inayoeleweka.

Obama Kuwasili Nchini Tanzania Julai Mosi

 
Wakati Ikulu ya Marekani ikitangaza kuwa Rais Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia Julai Mosi hadi 3, Serikali ya Tanzania imesema ujio huo utasaidia kuinua uchumi kutokana na kufaidika na uwekezaji na misaada mbalimbali.
Rais Obama anatarajiwa kuzitembelea Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Taarifa ya Ikulu ya Marekani iliyotolewa na Ubalozi wa nchi hiyo nchini, inasema Rais Obama atazuru Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, ikiwa ni moja ya sehemu ya kuimarika uhusiano baina ya nchi yake na bara la Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma alisema ziara ya kiongozi huyo inatarajiwa kuinufaisha Tanzania maeneo ya biashara na uchumi.
Rais Obama ambaye ana asili ya Kenya ambako anatoka baba yake mzazi, baada ya kuchaguliwa kushika madaraka nchini mwaka 2009, alimwalika Rais Kikwete akiwa kiongozi wa kwanza kwenda Marekani kujadiliana masuala mbalimbali.
Ziara yake ya kwanza kwa bara la Afrika aliifanya nchini Ghana ambako alihutubia Bunge.

P-funk Majani anaamini Profesa anaweza kuwa mbunge baada ya kujiunga na CHADEMA

 

Jana ilikuwa ni siku nzuri kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kumpokea mwanachama mpya Joseph Haule a.k.a Profesa Jay aliyekabidhiwa kadi ya Chama na mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu na John Mnyika.
...Read Full Story »

Rihanna haitaji kuliziba pengo la Chris Brown kwa sasa, ‘She’s not thirsty’

 

The Diamonds hit maker Rihanna anahitaji nafasi na muda wa kutosha kufanya mambo yake kivyake baada ya kuachana na Chris Brown.

Kwa mujibu wa Hollywoodlife rafiki wa karibu wa mrembo huyo amesema hajafocus katika kutafuta boyfriend ama mtu yeyote kwa kuwa hana
...Read Full Story »

List nzima ya washindi wa Billboard Music Awards 2013,Ulikuwa usiku wa aina yake kwa Justin Bieber na Tailor Swift



May 19 mwaka huu kulikuwa na tukio kubwa katika ulimwengu wa muziki ambapo tuzo za Billiboard zilitolewa kwa wasanii mbalimbali, Justin Bieber na Tailor Swift ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri na kuondoka na tuzo kadhaa.

...Read Full Story »

Roma mkatoliki ampigia debe Fid Q kwenye tuzo za Kili



Mshindi wa tuzo za kili kwa mwaka jana Roma Mkatoliki anaefanya kazi zake nyingi Tongwe Records chini ya Producer J-Ryder, amempigia debe mkali wa mashairi na flow toka Rock City Mwanza Fid Q ili aweze kuchukua tuzo kadhaa za muziki zinazotolewa na Kilimanjaro (Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013).

VURUGU ZA MTWARA ZASABABISHA BUNGE LIAHIRISHWE....!!


Spika wa bunge , Anne Makinda ameahirisha Bunge kutokana na hali ya Mtwara na ameiagiza serikali kuwa kesho wawasilishe taarifa bungeni kuhusiana na hali hiyo.

Makinda ameitisha kamati ya uongozi ili kuona kama wanaweza kutuma kamati ya Bunge kesho kwenda huko.

WASTARA RUKSA....... KUOLEWA


UWOYA, JOHARI KUZURU SAUZI....!!!

Irene Uwoya.
MASTAA wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya na Blandina Chagula ‘Johari’ wametimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwenda kurekodi filamu. Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni kwa njia ya simu akiwa nchini humo, Uwoya alisema wamekwenda nchini humo kurekodi sinema ambayo Watanzania wataitambua ikikamilika. Pia wataunganisha na ziara ndefu katika nchi mbalimbali barani Afrika zikiwemo Namibia, Ghana, Lesotho na kwingineko kujifunza soko la filamu.
 
Blandina Chagula ‘Johari’.
“Tupo huku na Johari lakini tutakuwa na ziara ndefu sana ya nchi mbalimbali za Afrika kwa ajili ya kulisogeza soko letu la filamu na kujifunza jinsi wenzetu wanavyofanya katika filamu zao,” alisema Uwoya.

AZAM MARINE WALETA MELI MPYA KALI ILE MBAYA, INAITWA KILIMANJARO IV

 Muonekano wa Kilimanjaro 4
KAMPUNI ya Azam Marine, inaleta boti mpya ya Kilimanjaro 4, ambayo inatarajiwa kuwasili nchini nchini, kuanzia mwishoni wa mwezi huu, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 700 na kutumia muda wa dakika 70 kwa safari moja ya kati ya Zanzibar na Dar es Salaam. Hii ni boti mpya kabisa katika muendelezo wa boti za Kilimanjaro, ambayo itakidhi mahitaji ya wasafiri wa eneo hili kwa kuwa inabeba sifa zote, ambazo ni Usalama, Kasi zaidi na Unadhifu. Kaa tayari kwa mzigo mpya kutoka Azam Marine.

MASHABIKI NCHINI KENYA WAMZOMEA MR NICE HUKU WAKIMUITA MAC MUGA, HIVI NDIVYO ILIVYOKUA


Mtandao wa ghafla kutoka Kenya umeripoti kuwa, msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa Iclub, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.


inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakua kama alivyotarajia. pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale, lakini Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidaikuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na magement yake.

inasemekana mashabiki walipata kichekesho kipya pale ambapo Mr Nice aliponyanyuka na kusema " Hamnilipi mimi nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi" baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo  wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka

PAPA FRANCIS AKIRI KUPITIWA NA USINGIZI WAKATI IBADA IKIENDELEA..Angalia VIDEO


Papa Francis I wakati wa Ibada hiyo.
Papa Francis amekiri kusinzia wakati akisali mwishoni mwa siku ndefu, lakini alisema anafikiri Mungu 'ameelewa'.
 
Baba Mtakatifu huyo alikuwa amesimama mbele ya watu 200,000 waliokusanyika pamoja kwenye Viwanja vya Mtakatifu Petro pale alipotoa maoni ambayo hayakupangiliwa kuanzia kutoka kumbukumbu za bibi yake, uamuzi wake wa kuwa Padri na rushwa katika siasa.
Akisababisha vicheko kutoka kwa umati huo, alifafanua
jinsi anavyosali kila siku mbele ya madhabahu kabla ya kwenda kulala.
"Wakati mwingine nalala, kazi hiyo ngumu ya siku hukufanya ujikute umelala, lakini Mungu anaelewa," alisema.
Akiwataka Wakatoliki kuongeza juhudi kusaidia mafukara na wenye mahitaji katika jamii alisendelea: "Kama tukijitoa, tutakuta umasikini.
Leo, inaniuma kuzungumzia, kukutana na mtu asiye na makazi ambaye amekufa kutokana na baridi, sio habari.
"Leo, habari ni kashfa, hiyo ndio habari, lakini hao watoto wengi ambao hawana chakula - hiyo sio habari.
"Hili ni kaburi. Hatuweza kubweteka kirahisi tu wakati mambo yakiwa namna hii."
Miongoni mwa umati huo, ambapo wengi wao tayari wanajihusisha na kazi za kujitolea, walimkatiza mara kwa mara kwa makofi.

source zero99

MAAJABU YA MTOTO ALIYETESWA NA WAZAZI WAKE MBEYA NA KUFUNGIWA NDANI MIAKA 2....!!



Moto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba  yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha.
Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutete meka migu tu 


Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena


 
Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana


Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana


Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo


Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza


Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani


Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo.


Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo.


VITUKO: ANGALIA VIDEO YA MKENYA ANAYELIA BAADA YA OBAMA KUPANGA KUJA TANZANIA NA KUIKACHA KENYA..!!



 

Angalia hiyo video “Obama skips Kenya; a frustrated Kenyan responds” Jamaa amenichekesha. Kamuahidi mpaka kumpa kuku

ANGALIA VIDEO YENYEWE HAPO CHINI 
Popout

HATARII....TUNDU LISSU NA ANNE KILANGO NUSURA WACHAPANE MAKOFI NJE YA BUNGE..TAZAMA PICHA




 


Baada ya Bunge kuahirishwa jana, nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri baina ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu
Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu.

 
Maneno hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia Lissu.

TAZAMA JINSI FLAVIANA MATATA ALIVYOSHIRIKI MISA YA KUWAKUMBUKA WAHANGA WA AJALI YA MV BUKOBA.



flaviana na babaake
Flaviana Matata akiwa na Baba yake mzazi katika Misa ya maombolezo ya Ajali ya MV Bukoba ambapo Flaviana alimpoteza Mama yake mzazi, Igoma,Mwanza
flaviana
Flaviana Matata akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya kuomboleza katika Makaburi ya Igoma Mwanza walikozikwa baadhi wananchi walopoteza maisha yao miaka 17 iliyopita.
Gonga continue reading kuendelea..

waombelezaji
Flaviana Matata akiwa na marafiki na baadhi ya waombolezaji waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo.

SIMBA YAMPANDISHA NGASSA MAHAKAMANI, HIKI NDO SIMBA WALICHOKISEMA. SOMA HAPA



UONGOZI wa Simba umechukua uamuzi wa kumpandisha kizimbani kiungo mshambuliaji, Mrisho Ngassa kutokana na uamuzi wake wa kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga.
 Mrisho Ngassa akikabidhiwa jezi bada ya kujiunga na Yanga.
Ngassa aliyekuwa akiichezea Simba kwa mkopo kutoka Azam FC, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga lakini Simba wamesema walishasaini naye mkataba wa mwaka mmoja.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa, Msimbazi wameamua kufanya mambo yao kimya na wameamua kutumia mahakama ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
“Hakika sasa tumeona suala hili si la kufanya kama filamu, maana wenzetu (Yanga) pamoja na Ngassa wameamua kutufanyia uhuni. Wachezaji wanataka kufanya Simba ni kama sehemu ya kuchota fedha na kuondoka.
“Kitu kibaya zaidi tumegundua system (mfumo) ya soka imekuwa ikiwalinda sana kutokana na ushabiki mkubwa uliopo katika kamati zilizo chini ya TFF. Sasa sisi tumeona bora kuchukua hatua zaidi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
“Tutamfikisha Ngassa mahakamani, tutadai zaidi ya Sh milioni 200 kama sehemu ya kutaka fidia kutokana na mkataba tulioingia naye. Mkataba upo, msione tumekaa kimya mnaona kama hatuna cha kusema.
“Ila sasa tumeamua kufanya mambo kwa mfumo tofauti na leo (jana) usiku tutakuwa na mkutano kwa ajili ya kujadili kuhusiana na suala hili na tutajua lini rasmi apande kizimbani.

KAKA, DADA WANASWA WAKIDUU COCO BEACH, MCHEZO MZIMA ULIKUA HIVI!

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni. Usemi huu unakamilishwa na tukio la kunaswa kwa vijana wawili wenye undugu wa damu wakifanya mapenzi ‘wakiduu’ kando ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi!
 Vijana wawili wenye undugu wa damu baada ya kunaswa wakifanya mapenzi.
Imefahamika kwamba vijana  hao, kaka na dada (majina tunayo)  wamenaswa ‘wakiduu’ katika mapango yaliyopo kando ya Ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
TUKIO ZIMA
Tukio zima lilitokea mchana kweupe wa saa 9 na kudhihirisha habari za mara kwa mara zinazoeleza kwamba Ufukwe wa Coco umekuwa ukitumika kwa ufuska usiku na mchana.
Risasi Mchanganyiko lilinasa tukio hilo kwa kutumia mitambo maaalum iliyoelekezwa kando ya bahari.
Wawili hao walinaswa tangu walipokuwa wakiingia katika ufukwe huo na kuwafuatilia nyendo zao, hatua kwa hatua.
 ...Dada akiwa kaduwaa baada ya kukutwa akivinjali na kaka'ake.
DEMU ALIKUWA AKIZINGUA
Haikufahamika mara moja kama wawili hao walikuwa na makubaliano ya kwenda kuduu katika ufukwe huo au la, lakini kwa mbali ilionekana kama vile dada mtu alikuwa akizingua kwenda kutenda dhambi hiyo.
Picha za video zilizonaswa, zinamuonesha dada huyo akionekana kutoa upinzani pale alipokuwa akishikwashikwa na kaka yake.
Alionekana kama vile hakuwa tayari kwa mchezo huo.
Hata hivyo, kaka mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23-26 alikuwa akilazimisha kitu fulani ambacho kilionekana dhahiri kupitia kamera zetu.
Ni kama vile hawakuwa na makubaliano na kile walichokuwa wakienda kukifanya.
Mara kadhaa dada huyo alionekana kumkwepa kaka yake na alikuwa akijiondoa karibu yake pale alipomlazimisha kutaka kumfanyia kitu kisichokuwa cha kawaida.
 ...Kaka akicharuka baada ya kunaswa akiduu na dada'ake.