Tuesday, May 21, 2013

Dr. Slaa amuonya vikali Spika Anne Makinda




 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyohudhuriwa na maelfu ya watu jana katika maeneo ya Ngalangala, Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. “Moja ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si vinginevyo.

Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze nini kisemwe. Hakuna,” alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Alisema kuwa baada ya mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata moja.

Source:Nipashe Jumanne.

Monday, May 20, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 21.03.2013


DSC 0043 f478a

DSC 0047 b993f

MATUKIO BUNGENI WAKATI WA UWASILISHAJI WA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

 Mbunge wa Ubungo Mhe.John Mnyika akizungumza na mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ndani ya ukumbi wa Bunge leo. IMG_1451IMG_1416Mbunge wa Mafia  Mhe. Abdulkarim Shah akiuliza swali la nyongeza bungeni IMG_1438Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe.  Adam Malima, akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa ndani ya ukumbi wa Bunge leo.IMG_1475Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.  Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na Naibu wake Mhe. Amos Makalla bungeni kabla ya kusomwa kwa bajeti ya Wizara hiyo. IMG_1500 
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara akiwasilisha hoja bungeni leo

FLAVIANA MATATA KUSHIRIKI KATIKA MISA YA KUMBUKUMBU YA MV BUKOBA

matata

Na Mwandishi Wetu
Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata leo atashiriki katika misa maalum ya kuwakumbuka watanzania waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba mwaka 1996.
Misa hiyo itafanyika kwenye eneo la makabuli ya kumbukumbu ya MV Bukoba ambapo Flaviana alipoteza mama yake mzazi na kaka yake katika ajali hiyo.
Mwaka jana, mwanamitindo huyu kupitia shirika lake la Flaviana Matata Foundation alitoa msaada wa maboya yaani vyombo vya kuokoa maisha majini (life vests) 500 kwa mawakala wa meli ya serikali yaani Marine Services Ltd ikiwa ni nja moja ya kujaribu kusaidia usalama majini.

Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM) ataka JamiiForums IFUNGIWE NA SERIKALI



Akiwa katika kipindi cha Jambo kikirushwa toka Bungeni akiwa na Mbunge wa Kasulu bwana Machari.

Mh. Machali kausifia mtandao wa JF kuwa unapendwa na chanzo kizuri cha habari kwa Jamii hasa Tanzania na kama mkombozi kwa habari

Cha kusikitisha sana Bwana Alhaj Juma Nkamia Kadai ni mtandao ambao hauna sifa ya kuitwa mtandao wa kijamii kwani unaandika uwongo na mambo ya kufikirika na utashi wa mtu

Anadai anajua lazima tumwandike na hataacha kusema. Anadai kuwa serikali inadai kuwa haiwafahamu wanaoandika utumbo katika mitandao kama jamii forum lakini anahoji iweje kama jamii forum kuna matangazo ya biashara na ni wazi kuwa wamiliki wake wanafaamika kwanini hawachukuliwi hatua?

RAIA WAGOMBANIA MAFUTA BAADA YA LORI LA MAFUTA KUPINDUKA MBEYA...!!

WAKAZI WA MLIMA NYOKA MKOANI MBEYA WAKIWA NA PILIKA KUELEKEA KUCHOTA MAFUTA BAADA YA GARI HILO KUPINDUKA.

SHUHUDIA WAKAZI WA MLIMA NYOKA WAKIWA WANAGOMBANIA MAFUTA

GARI LA KAMPUNI YA LAKE OIL BAADA YA KUPINDUKA




KILA MKAZI YUPO BIZE NA MAFUTA







HUYU NDIE BINTI ALIYETOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI

Msichana mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.


Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa.

Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.

Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.

Ushabiki: Afande Sele agoma kula siku 2 baada ya Simba kufungwa

 
King Selemani ama Afande Sele kutoka mji kasoro bahari Morogoro ni moja ya watu wanaoonekana kuwa ‘addicted’ na ushabiki wa soka kiasi cha kushindwa kuvumilia maumivu ya kufungwa kwa timu anayoishabikia, Simba kitendo kilichompelekea asuse kula toka Jumamosi.

Akizungumza na Suddy Brown katika segment maarufu ya U Heard kupitia XXL ya Clouds FM, mke wa rapper huyo mkongwe Mama Tunda, amethibitisha kuwa mumewe amegoma kula toka siku ya mechi. Mbaya zaidi kwa Afande ni kuwa Mama Tunda na binti yao Tunda ni mashabiki wa Yanga hivyo wao na Selemani Msindi ni mashabiki wa timu mbili pinzani, hatupati picha humo ndani panavyokuwa ikifungwa timu anayoshabikia baba wa familia!. Minuno ya hatari bila shaka. Pole Afande.

SUGU AMUUNGA JAYDEE BUNGENI, ASHANGAZWA NA SERIKALI KUWA KIMYA KATIKA MGOGORO WA JAYDEE NA CLOUDS FM.

Waziri Kivuli wa  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi akisoma hutuba ya kambi ya upinzani hivi punde amesema kwamba baadhi ya vyombo vya habari vikiwamo vituo vya redio vimekuwa vikiwanyonya wasanii nchini na kusababisha kuwa maskini.

Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesema bungeni kwamba hivi sasa kuna mgogoro mkubwa kati ya Lady Jay Dee na Radio Clouds FM, lakini serikali imekaa kimya mpaka sasa.

"Serikali imekaa kimya haitatui matatizo ya wasanii, hivi leo Clouds FM haipigi muziki wa Lady Jay Dee, tunakwenda wapi, chama cha wasanii ambacho ni halali
kimetaifishwa na kuundwa kampuni ya kusimamia shughuli za wasanii, lakini kwa malengo ya kuwanyonya," amesema Sugu.

Kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya Lad Jaydee na Clouds FM, Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini amewataka wasanii Tanzania kuacha uwoga na kutetea haki zao.

BAADA YA KUDAIWA KUA KAFULIA, HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MB DOG. SOMA HAPA




Hit maker wa ngoma isiyochuja masikioni ‘Si uliniambia’ MB Dog ameushangaa mfumo wa muziki wa Tanzania akilinganisha na mfumo wa muziki wa nchi kadhaa alizozitembelea na kikubwa alichokiona ni kwamba Tanzania hakuna ‘Respect’ kwa wasanii waliotangulia ama waliofanya vizuri na sasa wamenyamaza.

MB Dog amefunguka katika exclusive interview aliyofanya na leotainmenttz kuwa kwa nchi nyingine alizotembelea wasanii waliofanya vizuri miaka flani ya nyuma halafu wakanyamaza hupewa heshima hata kwenye matukio ya kimuziki tofauti kabisa na Tz ambapo aliyepo mbele ndo yupo na aliyemnyamaza hayuko kwenye hesabu.
“Yaani system ambayo mimi naiona ambayo iko juu sana kwa wenzetu, kitu kikubwa kwanza ni respect ya watu ambao waliotangulia na wanaofuata, unajua hapa muziki wa kitanzania kitu cha kwanza yaani aliyekuwepo mbele ndiye yupo, aliyenyamaza basi hayuko kwenye hesabu.

CHEKI PICHA ZA KILICHOJIRI USIKU WA KUMTOA MAMA YEYOO NA NJE BOX NDANI YA MAISHA CLUB

 Weusi jana walipiga show iliyopewa jina la "Usiku wa kumtoa mama Yeyoo Nje Box" kwenye ukumbi wa New maisha  club jijini Dar es Salaam,G nako,Nikki wa pili,Joh Makini,Lord Eyez,Peter Msechu, Ben pol walikuwa ni miongoni mwa waliotoa burudani..


PICHA MBALIMBALI ZA SUGU NA WAGENI WAKE BUNGENI LEO


Profesa Jay,Lady JayDee na SUGU
VINEGA wakiwa na lady JayDee
Peenlawyer na wageni wengine wa SUGU mjengoni leo
Lady JayDee,Pof Jay na Peenlawyer
Mh.SUGU

WEMA SEPETU APATA DILI LA MAMILIONI, PICHA NA STORY HIZI HAPA



Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amepata mchongo wenye pesa ndefu kutoka kampuni ya nywele ya Darling Hair Tanzania. 72b3721cc13c11e29bea22000a1f90d2_7
Kwa mujibu wa meneja wake, Martin Kadinda mkataba huo utamfanya Wema awe staa mwenye thamani kubwa zaidi Tanzania ingawa amesema si kawaida yao kutaja kiasi cha fedha.
1e5afc9ec13c11e2987d22000aaa0a97_7
Deal hiyo itamuonesha Wema akiwa kama msemaji na sura wa Darling Hair Tanzania.
CHANZO : BONGO5.COM

Hiki ni kipande cha hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni,iliyo SABABISHA BUNGE KUAHIRISHAASUBUHI,Isome na uielewe

MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA  JOSEPH O. MBILINYI (MB)

KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA
MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA,
UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA
WA FEDHA 2013/2014
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya
kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Dira ya Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa
lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye
uwezo na malezi bora, linathamini
utamaduni wake na linakuwa mahiri
katika michezo ifikapo mwaka 2025.”
Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni
‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa
kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari,
kuwawezesha vijana kiuchumi na
kukuza utamaduni na michezo kwa
umma kwa maendeleo ya kijamii na
kiuchumi.’
Mheshimiwa Spika,
Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa
kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa
katika maandiko ya kisera ya Wizara.
Badala yake, chini ya usimamizi wa
Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa
taifa lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri
juu ya matendo ya watawala. Tanzania
imegeuka kuwa taifa linalofungia
magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu
na matumizi mabaya ya madaraka
miongoni mwa viongozi, watendaji na
watumishi wa Serikali hii ya CCM.
Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi
wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa
taifa linaloteka nyara wanahabari,
kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na
meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia
tindikali na hata kuwaua.

Loveness Diva"Hivi Wewe Zitto Kabwe Unadhani unastahili Kweli Kuwa Raisi wa Tanzania?

 Baada  ya  kutangaza  kumpiga  chini  Mh.Zitto Kabwe, Loveness  Diva  ameamua  kumchokonoa  tena  kwa  kumkejeli  kuhusu  uamuzi  wake  wa kugombea Urais.....

Huu  ni ujumbe wake aliouweka instagram:

 ".Ivi  kwa akili yako unadhani  unastahili  kweli  kuwa Rais mteule wa taifa  hili....??

BREAKING NEWZZZ : MSIGWA APEWA DHAMANA

MBUNGE WA CHADEMA IRINGA MCHUNGAJI MSIGWA HATIMAYE AMEPEWA DHAMANA SASA HIVI NA WENGINE 60 WALIOLETA VURUGU KUBWA SANA JANA MJINI IRINGA NA KUHARIBU MALI NYINGI SANA ZA WANANCHI

ASKARI MAGEREZA MWENYE CHEO CHA KOPLO ANUSURIKA KIPIGO BAADA YA KUDAIWA KULAWITI VIJANA MOROGORO. by Jackson Audiface


Askari wa jeshi la magereza wakionyesha uhidari wao katika gwaride, picha hii ni ya maktaba haiusiane na tukio hili.
ASKARI magereza mwenye cheo cha Koplo amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kubainika kuwalawiti kwa siku moja vijana wawili wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 20.
Tukio la kuwalawiti vijana hao linadaiwa kufanywa na askari huyo kati ya majira ya saa 7.00 mchana  na saa 2.00 usiku katika moja ya nyumba za kulala wageni (jina limehifadhiwa) iliyoko mtaa wa Mafisa manispaa ya Morogoro.
Akisimulia mkasa huo, Meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni jina tunalo alisema kuwa imekuwa ni desturi ya askari huyo kwenda na vijana wa kiume katika nyumb

Alisema kuwa siku ya tukio askari magereza huyo alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni majira ya saa 7.00 mchana akiwa amempakia kijana mmoja katika pikipiki yake na kabla ya kukabidhiwa funguo ya chumba namba 202, mhudumu wa nyumba hiyo alimwambia askari magereza huyo kuwa masharti ya nyumba yao hayaruhusu watu wa jinsia mmoja kukaa chumba kimoja.

JK: MNAOTAKA URAIS 2015 ANZENI KUPITAPITA.

 
MWENYEKITI WA CCM DK JAKAYA KIKWETE.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amefungua milango kwa kuwataka baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowania urais mwaka 2015 kuendelea na mchakato huo.
Rais Kikwete amewatahadharisha watu hao kuendesha kampeni zao kwa ustaarabu pasipo kuibua chuki wala kujenga makundi ambayo alisema ni hatari kwa kuwa yanaweza kukipasua chama.
Rais Kikwete aliyasema hayo katika mkutano ndani wa wabunge wa chama hicho uliofanyika jana katika ukumbi wa CCM (white house) mkoani hapa.
Mkutano huo ambao ulianza saa 3.00 asubuhi ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya taifa ikiwamo utekelezaki wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho katika majimbo na ahadi mbalimbali za viongozi wa taifa.
Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya ukumbi huo kilieleza kuwa Rais Kikwete aliwataka wanachama wenye nia ya kugombea urais kuwa na tahadhari na watu aliowaita vishoka wa siasa.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete alisema watu wa aina hiyo wana tabia ya kula huku na h
uku kwa kujiingiza katika kambi zaidi ya moja.





“Tuangalie makundi ya urais 2015 yasishambuliane kwa kuvunja chama, wenye nia hiyo ya kugombea waendelee na mikakati yao kujenga chuki kwa makundi mengine.


“Katika hatua hiyo, pia mkumbuke kuwa katika kambi hizo za urais zinatakiwa kujitizama wao na wafuasi wao maana wafuasi wengine hawaaminiki, ” alisema Rais Kikwete.


Kwa mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa ajenda alizokuwa nazo Rais Kikwete ni pamoja na suala la urais na utendaji wa wabunge majimboni.

TANGAZO KUTOKA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUHUSU KUFUNGULIWA CHUO


CHUO CHA UHASIBU ARUSHA
TAARIFA YA KUFUNGUA CHUO
Chuo cha Uhasibu Arusha kinawatangazia Wanafunzi wote wa kozi 
za ngazi ya Cheti hadi Stashahada ya Uzamili kwamba chuo 
kitafunguliwa siku ya Alhamisi tarehe 23 Mei, 2013.
Kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 27 Mei, 2013 kutakuwa na zoezi la 
usajili katika lango kuu la kuingia chuoni kwa kuzingatia masharti
yafuatayo:
1. Kila Mwanafunzi aliyeomba upya kujiunga na chuo anapaswa 
kuonyesha kitambulisho chake cha chuo.
2. Kila Mwanafunzi aje na risiti au “Bank pay in slip” ya 
kuonyesha malipo ya karo na fedha zote anazodaiwa na chuo.
3. Kila Mwanafunzi anapaswa kuingia mkataba mpya na Chuo. 
Mkataba huo unapaswa kusainiwa kabla Mwanafunzi 
hajasajiliwa.
4. ANGALIZO: Hakutakuwepo na usajili baada ya tarehe 27 Mei,
2013.
Mkuu wa Chuo

ANGALIA PICHA ZA MBUNGE MSIGWA ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA MCHANA

 Mbunge  Msigwa akishuka katika gari ya  polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana  huu
 Mbunge  Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea  chumba cha mahakama
 Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya  kufikishwa mahakamani