Habari
kamili zilizonaswa na waandishi wetu ni kwamba mwanaume aliyetajwa
kwa jina la Baba Asha alidai kumfumania rafiki yake wa karibu, Baba
Tony akiwa gesti na mkewe (jina linahifadhiwa), tayari kwa kuvunja naye
amri ya sita.
Tukio
hilo la aibu ya milenia lilijiri katika nyumba ya kulala wageni ya
Pumzika iliyopo maeneo ya Msimbazi Center, jijini Dar ambapo mara baada
ya kumtia mikononi ‘mwizi’ wake ambaye mbali na urafiki pia ni
majirani, ndipo akamchakaza sura vibaya na kumsababishia kuvuja damu.
Habari
za kina zilidai kuwa mke wa Baba Asha alikuwa bafuni akioga, mara
ukaingia ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye simu yake ya kiganjani, ndipo mumewe
akachukua kilongalonga hicho na kuufungua ujumbe huo.
Ilidaiwa kuwa mume alitaharuki kukutana na ujumbe uliokuwa ukimtaka mkewe kwenda Pumzika Guest House kukutana na jamaa huyo.
Iliendelea
kudaiwa kuwa Baba Asha hakuyaamini macho yake, akausoma tena ule
ujumbe na ndipo akagundua sms nyingine nyingi, vocha na fedha za
mtandao alizokuwa akitumiwa mke wake kutoka kwa Baba Tony.
Chanzo
kilidadavua kuwa baada ya kugundua mchezo mzima, Baba Asha akatulia na
kumsubiri mkewe atoke bafuni ili kuliweka sawa suala hilo.
Ilifahamika
kuwa mke aliporudi kutoka kuoga, mume hakuonesha dalili zozote,
alichokifanya ni kumwita mkewe na kumwambia kuwa achague moja,
kufungasha kilicho chake, aondoke nyumbani kwake au amwekee jamaa mtego
anaswe ili ajue mke wa mtu ni sumu.
Jibu lilikuwa rahisi kwani alikubali kuweka mtego ili amnase mbaya wake ndipo atamsamehe.
Ilifahamika
kuwa ilipita wiki moja kimyakimya kwani mara ya kwanza Baba Tony
alichezwa na machale, alipofika kwenye gesti hiyo na kumwona mtu
anayemfahamu, alimwambia yule mwanamke waahirishe.
Habari
za uhakika ni kwamba wiki iliyopita, Baba Tony aliingia kwenye kumi
nane, akajaa mzimamzima kwenye mtego wa fumanizi uliowekwa na Baba Asha
na mkewe.
Mara
baada ya kuona mwanaume mmoja (Baba Asha) akiwa na askari kwenye gesti
hiyo akihaha, king’ora kililia kwenye akili ya mwandishi wetu ambaye
hakufanya makosa, akamfuata mfumaniaji kwa nyuma hadi aliporuhusiwa
kumfuata mkewe chumbani.
Chumbani mtiti ulikuwa mkubwa ambapo Baba Tony alikutwa kama alivyozaliwa huku mke wa mtu akiwa bado hajavua na ndipo mtiti ukaanza.
Katika
purukushani, Baba Asha alimpa kibano ‘mwizi’ wake hadi akamchana usoni
na kumng’oa meno ya mbele, jambo lililosababisha kutokwa na damu
nyingi.
Kama
hiyo haitoshi, ili kuthibitisha kuwa mke wa mtu ni sumu, Baba Asha
alimchoma jamaa huyo bisibisi kwenye makalio hadi askari alipoingilia
kati na kumchukua mtuhumiwa kisha akamtoa nje.
Wakiwa
nje ya gesti hiyo, Baba Tony aliomba kujisafisha damu na baada ya hapo
alipigwa pingu tayari kwa kupelekwa Kituo cha Polisi, Pangani,
Ilala...
No comments:
Post a Comment