"Kabla ya mazingaombwe ya CD
ya Rwakatare hali ya
ndani ya Chadema ilikuwa haileweki, kumbuka
ndiyo kwanza walikuwa wametoka kwenye suala la akina Shonza na watu
makini wanaofuatilia duru za kisiasa nchini walikuwa bado wanapima suala
hilo uzito wake na madhara yake kama yangetokea.
Ccm sijui kwa
kutokuwa na mipango makini au kukurupuka, au kiwewe wakaingia na CD!
Chadema sijui kwa umakini au kwa bahati wakalifanyia kazi vizuri sana.
Kwanza Mbowe alilibeba vizuri sana kwenye mikutano ya kuzindua kanda,
nakumbuka mikutano yake ya Mbeya na kanda ya ziwa alilieleza kwa hisia
na kuwajaza watu hasira kwa kuwaaminsha kwamba Ccm inateka watu na
kuwaumiza kiasi kile kwa faida za kisiasa.
Kiboko yao alikuwa ni
Marando Mabere alipowaumbua watekaji, na kama kawaida yao Ccm wakaja na
utetezi 'kipumbavu' eti kuingilia mawasiliano ya mtu ni kosa! Hivi huu
ni upungufu wa umakini kiasi gani?????? Badala ya kuwaondoa watuhumiwa
katika tope hili, eti kuingilia mawasiliano ya mtu ni kosa!!!!
Likafuata
suala la kufukuzwa wabunge machachari wa Chadema bungeni, hili nalo
kulikuwa na jinsi ya kulikwepa maana Spika wakati anasubiliwa awaondolee
adhabu au kuikazia angekuja na kusema nimewasamehe na ninawaonya kwa
kosa hilo. Angekuwa ameliuwa suala kisiasa, badala yake akakazia hukumu
na vijana wakaingia mitaani wakaomba huruma ya wananchi na kweli
wakaipata. Ukidadisi maoni ya watu wanasema baada ya kuua uhuru wa
vyombo vya habari na mahakama sasa wameliua bunge.
Kiwewe
kikaendelea kwa suala la Lema, ujinga, ujinga, ujinga juu ya ujinga!!!!
Chama
hiki kina washauri? Washauri wenyewe ni kina Nape na Mwigulu? Kama ni
hao chama kimefilisika kiasi hicho?
Akina Mangula na Kinana wanakuwa
wapi wakati chama kinafanya makosa ya kijinga na kitoto namna hii?
No comments:
Post a Comment