Jana
CLOUDS FM iliripoti kuhusu kushamiri kwa Biashara ya Ngono katika
Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na jinsi serikali
inavyolishughulikia tatizo hilo linalokua kwa kasi....
Wakihojiwa
kwa nyakati tofauti, baadhi ya wasichana wanaojishughukisha na
biashara hiyo wameelezea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika
kazi hiyo hususani nyakati za usiku.
Wakizungumzia adha
wanazokutana nazo Wasichana hao wamesema kuwa licha ya kukabiliwa hali
ngumu ya maisha iliyopelekea kuingia katika biashara hiyo, bado wamekuwa
wakikutana na matukio mabaya ikiwemo kukamatwa na kuingiliwa kinguvu na
baadhi ya watu wanaojitambulisha kwao kuwa ni askari wa Polisi jamii.
Mbali
na hilo Wasichana hao wamesema hali ngumu ya Maisha imekuwa ikiwalazimu
kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanapokuwa kwenye Hedhi, pasipo
kujali hatari ya kukumbwa na maradhi yoyote.
Hivi karibuni Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilitangaza mpango wa kuwaondoa wasichana
wamaojishughulisha na Biashara ya ngono mitaani na kuwashtaki kwa mujibu
wa Sheria ya makosa ya uvunjifu amani na ukiukwaji wa maadili.
Wakizungumza
baadhi ya wadau kutoka mashirika na Taasisi mbalimbali za kutetea haki
za Binadamu nchini, ambapo kituo cha Sheria na haki za Binadamu pamoja
na taasisi ya kutetea haki za Binadamu ya Chuo Kikuu cha Tumaini,
kimesema kuwa kitendo cha kuwakamata wasichana hao hakiwezi kuwa
suluhisho la kutokomeza Biashara ya ngono nchini.
Eneo la
MANZESE Uwanja wa Fisi ni miongoni mwa Maeneo ambayo Jeshi la Polisi
kanda maalum ya Dar es salaam limeliainisha kuwa limekuwa likikithiri
kwa Biashara hiyo
No comments:
Post a Comment