Sunday, April 28, 2013

BEN POL AWA KIVUTO KILIMANJARO MUSIC AWARDS




MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye ameweza kujizoelea umaarufu kwa kupitia kazi zake Diamond Platnamu ameshindwa kuchomoza katika uteuzi wa kuania tuzo za muziki za Kilimanjaro (Kilimanjaro Music Awards 2013)

Msanii huyo ameshindwa kuchomoza tena kwa kipindi hiki huku msanii mwenzie Ben Pol akionekana kung'ara kwa kuteuliwa mara 6 katika vipengere tofauti tofauti kitu ambacho ni cha tofauti na miaka mingine iliyopita

Inawezekana hali hiyo imechangia na juhudi za msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya Ben Pol kwa kuongeza ubunifu kwa kazi zake pamoja na kujizolea mashabiki wengi kupitia nyimbo zake zenye ujumbe wa mapenzi

Ben Pol ambaye ameonekana kunga'ra katika uteuzi huo wa majina hali inayoonyesha kumsababisha kupata tuzo nyingi tofauti na mwaka jana ambapo aliweza kuteuliwa katika kipengere kimoja cha nyimbo bora ya R&B na kuweza kunyakua tuzo hiyo

Hali za tuzo hizo kwa sasa imeoneka kuwa tofauti kwa kuongezeka kwa vipengere vingi tofauti tofauti hadi kufikia vipengere 35 ambapo inaonyesha kutoa fursa kwa wanamuziki wa Tanzania kutambulika na kutambua kazi zao za muziki

No comments:

Post a Comment