Monday, April 29, 2013

RAISI OBAMA ATANIA KUHUSU UTATA WA JAY Z KWENDA CUBA KWENYE CHAKULA CHA JIONI NA WAANDISHI

 Ile dinner ambayo huwa inafanyika kila mwaka ndani ya Ikulu ya Marekani "White House Correspondents", imekuwa na idadi kubwa ya marejeo ya Hip hop, kuanzia jinsi ambavyo Obama alivyokuwa akiingia, ambapo aliigia na wimbo wa Dj Khaled "All I Do is Win" 
"Mnaonaje wimbo nilioingilia nao? aliuliza Obama, Rush Limbaugh, nilikuonya kuhusiana na hili.term ya pili, baby, tunabadilisha vitu kidogo.
Actually, washauri wangu, walikuwa na wasiwasi kidogo, kuhusu kuingia na wimbo wa Rap, alikubali Obama na kusema ilikua imezoeleka kuingia na wimbo wa kitamaduni.
Obama hakuishia hapo, aliendelea na kutiririsha utani, kuhusu kumpa go ahead Jay Z, kwenye utata uliotokea kuhusu safari ya Jay Z na Beyonce kwenda Cuba na pini jipya la Jay Z linamitaja Obama.
Vitu vingine viko nje ya uwezo wangu, kwamfano, huu utata uliopo kuhusu safari ya Jay Z na Beyonce kwenda Cuba, ni ajabu, nina matatizo 99 na sasa la Jay Z.
" hili ni rejeo lingine la HIp Hop" amesema Obama akirejea kwenye wimbo wa Jay Z "99 Problems" 
Wiki kadhaa zilizopita, Rais alijiweka mbali na safari hiyo ya Jay, kwa kusema kuwa hakuwa anaelewa chochote juu ya safari hiyo ya HOV na Beyonce kwenda Cuba.



No comments:

Post a Comment