Sunday, April 28, 2013

WALE WA TAMTHILIA FUATILIA STORY YA MARA CLARA HAPA

POSTER- Mara Clara
EPISODE YA 52 GARY AANZA KUMUONYESHA ALVIRA UNYAMA
Baada ya Amante kukosa ushahidi wa kutosha kwa Gary, sasa aamua kumfuatilia katika bishara yake mpya haramu ya dawa za kulevya ili apate sababu ya kumtupa jela Gary. Huku nyumbani kwa Alvira mahusiano yake na Gary yanathibitika baada ya Alvira kutamka mbele ya Amante na Gary kuwa hampendi Amante na bali anampenda Gary peke yake.
Gary anatoa maoni kwa Alvira “nikwanini tusimuondoe Amante duniani ili aache kutuingilia penzi letu?” Alvira anashtuka na kukataa kata kata na kumwambia Gary asijaribu kuingilia na kumdhuru Amante kwani huo ni ugomvi wao, na pia Amante bado ni mumewe wa ndoa. Alvira anaanza kuutambua moyo wa Gary kwa matendo anayoanza kumuonyesha.
Gonga continue reading kuendelea..

Gary anaanza kama kumlazimisha Alvira wanyonyane ndimi, pia ahamie kwa Alvira, lakini Alvira kwasababu malengo yake sio kuolewa na Gary ni kutafuta vidhibiti vya maovu ya Gary, hivyo anamwambia Gary asiwe na haraka ya mambo, muda utafika tu.
Huko kijijini Suzan anapata vipimo kuwa ni mjamzito, ujauzito unaosemekana kuwa ni wamumewe Gary. MARA adhamilia kabisaa kurudi nyumbani kwao, lakini Alvira anamsihi Suzan amzuie kwani huko mambo bado sii mazuri. Huku mjini Clara nae amerejea tena huku akiendeleza kumfanyia bibi yake ugaidi.
Mama yake Gary anapata nafuu ya kuweza kutembea japo kwa shida, hadi alikochimbia zile fedha za Gary. Akiwa bado anachimbua, mfanyakazi wake anaanza kumtafuta huku akisaidiana na CG,wanamkuta japo alikuwa bado hajazitoa.
Amante anajipanga yeye na wenzake ili kumfuatilia Gary katika biashara zake za dawa za kulevya, anafanikiwa kuchukua video kwa njia ya simu, lakini wenzake Gary wanashtukia kuwa kunamtu anawafuatilia, hivyo wanamwambia Gary. Amante akiwa bado ananyata kuondoka mara Gary anatokeza kwa nyuma yake na bastora na kusema “Amante leo sitokuacha, huwezi kuondoka”, Gary anampiga risasi na Amante kuanguka chini.
Nyumbani kwa Gary yeye na Clara wanafanikiwa kuzifukua zile pesa zilizokuwa zimefukiwa na mama yake. Amante afanikiwa kufikishwa hospitali, huku Suzan na MARA wafanikiwa kurudi na kufika hospitali kumuona Amante.
Gary anafika hospitali na kumkuta Suzan na MARA, anatoa bastora na kumnyoshea Suzan lakini Alvira na MARA wanamzingira Suzan kwa pamoja, mara Gary bado akiwa na hasira anawauliza “mnafikiri mtakimbia kwenda wapi?” anawaonyooshea bastora wote watatu. Huku Madaktari wanajaribu kumpiga shoti Amante ili azinduke lakini juhudi kama zinagonga mwamba hivi!
Mwandishi: Vikta Machota (Asili Yetu Tanzania)
To be continue..

No comments:

Post a Comment