
MAGHOROFA yaliyojengwa kandokando ya Mto Mlalakua na Ufukweni mwa Bahari ya Hindi yatabomolewa, hivyo kuzua mshtuko mkubwa kwa wamiliki.
Habari zaidi zinadai kwamba baadhi ya vigogo hao wamekimbilia mahakamani kufungua kesi ya kupinga nyumba zao zisiguswe wakati wengine wamekua wakitoa vitisho kwa waliopewa…
Na Waandishi Wetu
MAGHOROFA yaliyojengwa kandokando ya Mto Mlalakua na Ufukweni mwa Bahari ya Hindi yatabomolewa, hivyo kuzua mshtuko mkubwa kwa wamiliki.
MAGHOROFA yaliyojengwa kandokando ya Mto Mlalakua na Ufukweni mwa Bahari ya Hindi yatabomolewa, hivyo kuzua mshtuko mkubwa kwa wamiliki.
Habari zaidi zinadai kwamba baadhi ya vigogo hao wamekimbilia mahakamani kufungua kesi ya kupinga nyumba zao zisiguswe wakati wengine wamekua wakitoa vitisho kwa waliopewa mamlaka ya kuzibomoa.

Kutokana na ujenzi huo holela, wakazi wa Kawe kwa Malecela waliamua kumwandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka wakitoa malalamiko juu ya ujenzi huo.
Barua hiyo ambayo gazeti hili lina nakala yake iliyoandikwa Februari 20, mwaka huu ilieleza kwamba ujenzi wa nyumba hizo umekuwa ni kero kubwa kwani zimejengwa katika mkondo wa maji hivyo mvua inaponyesha inasababisha mafuriko kwa wananchi wengine.
Walidai kuwa nyumba nyingi zimejengwa katikati ya mto na wengine wamejaza vifusi kando ya mto unaopita karibu na nyumba zao, hivyo kusababisha mkondo wa maji kwenda kwa wananchi.
Waliendelea kusema kwamba vigogo hao ambao ni wavamizi baadhi yao wamekuwa wakitembea na bastola hadharani na kuwatishia maisha wale wanaodiriki kuzungumzia ujenzi wanaoufanya katika maeneo hayo.

Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Hifadhi ya Mazingira nchini (NEMC), Ignas Mchallo alisema:
“Wote waliojenga katika maeneo hayo watahamishwa kwa kufuata sheria kwani kuna wengine waliojenga kabla ya sheria ya mazingira ambayo inataka kuwepo kwa nafasi ya mita 60 toka mtoni au ufukweli,” alisema Mchallo.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema kwamba nyumba 73 zilizojengwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi, zitavunjwa na akazitaja kuwa ziko kwenye fukwe za Kawe, Mbezi na Msasani na kwamba ingawa zilijengwa kihalali baada ya kupewa hati, lakini sheria mpya hairuhusu nyumba hizo kuwepo.
No comments:
Post a Comment