Monday, April 29, 2013

MWANAMAMA WA CONGO ACHAGULIWA KUWA WAZIRI NCHINI ITALY.

.
Mwanamke wa kwanza mwenye asili ya kiafrika aitwae CECILE KYENGE KASHETU kutoka nchini CONGO DRC amechaguliwa kuwa Waziri nchini Italy, alizaliwa Agust 28 1964 na baadae aliolewa na Mwitaliano ambapo mpaka sasa ni Mama wa watoto wawili.
Alihamia nchini Italy mwaka 1983 na kuchukua uraia, alihitimu mafunzo yake ya Udaktari unaohusiana na madawa katika chuo cha Universita Cattolica del Sacro Cuore kilichopo Roma, baada ya kumaliza chuo makazi yake yalikuwa eneo moja liitwao Castelfranco Emilia Jimbo la Modena mkoa wa Emilia- Romanga akiwa anaendelea na kazi yake ya udaktari.
.
.
Mwaka 2004 alijiunga na mambo ya siasa katika chama cha PD yani Partito Democratico na alipata nyadhifa mbalimbali mwaka 2010 lakini february mwaka huu ndio alichaguliwa kuwa Mbunge kupitia chama chake cha PD, mwezi huu wa April 2013 ndio huyu mama amechaguliwa kuwa Waziri anaehusika na mambo ya kigeni.
.

No comments:

Post a Comment