Sunday, April 28, 2013

MIAKA 13 YA LADY JAY DEE KWENYE MUZIKI KUDONDOSHA BONGE LA PARTY

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika mwaka huu 2013, Inatimia miaka13 tangu nianze kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tukopamojanapia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea ku support muziki wa Tanzania nakunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyotevya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki. Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV. Shereheyamiaka 13 ya Lady Jay Dee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUT ambayo ina jumla ya nyimbo 10.

Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za Jay Dee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.

Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu awabariki

No comments:

Post a Comment