Saturday, April 27, 2013

PADRI WA PAROKIA YA IFUNDA AFARIKI KATIKA AJALI AKITOKEA MSIBANI NJOMBE.


     Hili ndilo gari ambalo  limesababisha  kifo cha paroko
             -------
PAROKO  wa kanisa la RC parokia ya Ifunda Alphonce Mhamilawa amefariki  dunia katika ajali mbaya ya gari  iliyotokea katika eneo la Sabasaba Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Mashuhuda  wa  ajali  hiyo wameueleza mtandao  huu  kuwa ajali  hiyo ilitokea  majira ya saa 2 usiku  wa  kuamkia  leo wakati paroko  huyu akitoka mkoani Njombe katika  shughuli  ya Mazishi

Mmoja kati ya mashuhuda  hao Bw  Saugo Ndemo  alisema  kuwa paroko  huyo alikuwa akiendesha gari dogo aina ya Toyota  Hilux (Pick Up) yenye  namba  za usajili  T434 APP mali ya Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Ifunda.

Ndemo  alisema  kuwa chanzo  cha ajali  hiyo ni Paroko  kuligonga gari aina ya Lori  kwa  nyuma na kuwa lori  hilo halikuweza  kusimama.

Alisema  kuwa  paroko  huyo alifia eneo la tukio baada ya  ajali  hiyo  iliyopelekea  kichwa  chake  kupasuka.

Mmoja kati ya askari  wa usalama barabarani ambae hakutaka  kutaja jina lake kwa  kuwa si msemaji  mkuu  wa  jeshi la  polisi alisema  kuwa  chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi.

Pia alisema kuwa lori ambalo paroko huyo aliligonga linasadikika  kuwa lilibeba mbao huku  likivutana na  lori  jingine na baada ya ajali  hiyo halikuweza  kusimama.

No comments:

Post a Comment