Sunday, April 28, 2013

TYRESE AOMBA RADHI 'VIBONGE'



Baada ya kutoa maoni makali dhidi ya watu wanene katika mahojiano na jarida la AllHipHop mapema mwezi huu Tyrese ameanza kuonyesha hali ya wasiwasi huenda akapoteza mashabiki wake kutokana na kushambuliwa vikali

Katika mahojiano msanii huyo aliwachana watu wanene akiwaita 'mabonge nyanya na wabaya' akiwaambia wafanye jambo kuondokana na hali hiyo

Muda mfupi baada ya kutoa kauli hiyo Tyrese aliingia katika ukurasa wake wa Twitter kuomba radhi kisha akaenda kwenye kipindi cha Tom Joyner Morning Show Aprili 23 kuomba radhi rasmi kutokana na maoni yake akiyaita 'Uchaguzi mbaya wa maneno ya kusema'

No comments:

Post a Comment