Saturday, April 27, 2013

MGANGA AELEZEA ISHU YA DIAMOND KUNG'ANG'ANIA MAITI YA BI.KIDUDE KWA NIA YA KUIBA NYOTA YAKE

Baada ya msiba wa Bi Kidude kumalizika, hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ alibaki peke yake na mwili wa marehemu chumbani kwa ajili ya kuchota nyota ya Bi. Kidude.
Leo tunaye Dr Salum Mkumba ambaye ataeleza kwa kirefu tafsiri ya kitendo alichokifanya Diamond.
Funguka: Dr Mkumba asalam aleikum, karibu ndani ya nyumba kubwa ya magazeti Pendwa Tanzania, Global Publishers Ltd.
Dr Mkumba: Waaleikum salaam, ahsanteni nashukuru. Mimi leo nina jambo ninataka niliweke sawa.
Funguka: Liweke sawa, sisi pamoja na wasomaji wetu wa Risasi Jumamosi tunakusikiliza.
Dr Mkumba: Nataka kuweka sawa juu ya suala la nyota, mtu akifariki huwa anakwenda na nyota yake sasa nimeshangaa kusikia Diamond alikwenda kuchukua nyota ya marehemu.
Funguka: Sasa Diamond alipobaki peke yake chumbani na mwili wa marehemu ilikuwa ina maana gani?
Dr Mkumba: Pale alikuwa anajaribu kujisafisha tu katika jamii, hakuna cha ziada.
Funguka: Unaposema anajisafisha, kwani amechafuka?
Dr Mkumba: Eee! Kwani hujui? Amenaswa na mke wa mtu hotelini, skendo za wanawake tofauti zimekuwa zikimtafuna kila kukicha.
Funguka: Unaposema alikuwa anajisafisha una kitu gani cha kushika mkononi?
Dr Mkumba: Surat Nnajimi Sura ya 39 imezungumza kwa kirefu ila tafsiri yake ipo hivi; hakuna anachokichuma mwanadamu kwa marehemu ila marehemu anategemea kuombewa dua na mtu mzima.
Funguka: Kwa hiyo ina maana vile alivyofanya Diamond ni kazi bure?
Dr Mkumba: Nakwambia hakuna cha maana zaidi ya kujisafisha.
Funguka: Sasa una mshauri nini Diamond?
Dr Mkumba: Amrudie mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada ya kweli.
Funguka: Vipi kuhusu suala la kujenga msikiti ambalo Diamond alitangaza kuwa ana mpango huo?
Dr Mkumba: Hapo ndiyo kabisa, ajenge tu lakini haisaidii kitu sababu ukijenga nyumba ya ibada inatakiwa utumie fedha ambazo umezipata kihalali katika njia safi.
Funguka: Kwani fedha zake hajazichuma kwa njia safi?
Dr Mkumba: Kiimani yetu ya Kiislam muziki siyo halali hivyo fedha anayoipata kwenye muziki haiwezi kuwa halali.
Funguka: Tunashukuru, karibu tena siku nyingine.
Dr Mkumba: Haya Ishallah!

No comments:

Post a Comment