Monday, April 29, 2013

KALI YA LEO: MARIO BALOTELLI AWAAMBIA MADRID WAKIMTOA DORTMUND BASI DEMU WAKE ATAKUWA HALALI YAO

Mario Balotelli anaweza akajiingiza kwenye ugomvi na mchumba wake Fanny Neguesha baada ya kuripotiwa kwamba ametamka kuwa ikiwa Real Madrid wataweza kubadili matokeo na kuwatoa Dortmund basi atawaaruhusu wachezaji wote wa kikosi cha Los Blancos kulala na mchumba wake huyo mwanamitindo mwenye asili ya Ubelgiji.



Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City ana uhakika Dortmund watafuzu kucheza fainali ya Champions League, na alikaririwa na magazeti ya AS na Marca akisema kwamba ikiwa Ronaldo na wenzie watafanikiwa kwenda Wembeley basi angemtoa sadaka mpenzi wake huyo kwa wachezaji wa Madrid.
‘Ikiwa Real Madrid watapita kwenda fainali ya Champions League, nitawaachia mchumba wangu alale nao wote!’

No comments:

Post a Comment