“Tunakubaliana
na kazi zao, lakini kusema ule ukweli, sisi abiria wenzao tulishangaa
sana, unajua kuonesha vitendo vya mahaba ndani ya ndege si utamaduni
wetu Wabongo,” alisema abiria huyo aliyekuwa akienda Mwanza kikazi.
Aliongeza kuwa, ilifika mahali baadhi ya abiria walitaka kuwafungukia
ukweli kwamba wanachokifanya si adabu hasa ikizingatiwa kuwa wao wana
majina makubwa katika burudani za Bongo. Kufuatia taarifa hizo na
kudakwa kwa picha zao, Amani liliwasaka watuhumiwa hao kila mmoja kwa
wakati wake ili kusikia kutoka kwao juu ya kufanya madudu ndani ya
‘pipa’. Kwa upande wake, Shilole alisema
kuwa mabusu ni vitu vya kawaida kwake ikizingatiwa Q-Chillah ni
mwanamuziki mwenzake kwa hiyo hakuna tatizo. “Jamani kwani mabusu
yana shida gani, yule (Q-Chillah) ni mwanamuziki mwenzangu na
tumezoeana. Yale yalikuwa ni mambo ya kawaida tu na utani, si
vinginevyo,” alisema Shilole. |
No comments:
Post a Comment