Kutokana na hali hiyo ya baadhi ya wabunge kukosa lugha na sera zenye tija wawapo bungeni baadhi ya wasanii wanaliona hilo ni moja ya changamoto inayosababisha watanzania kuzidi kuwa na hari ngumu ya kimaisha kwa kukosa watetezi wenye umakini
Mmoja wa wasanii hao akizungumza na jarida hili Ben Pol alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wabunge kutumia lugha ya matusi kwenye kujadili hoja na matokeo yake wanashindwa kupata muafaka wa wanayo yajadili
Alisema kuwa bunge limekosa muelekeo na ameacha kulisikiliza bunge hilo kwa sababu ya kukosa mueleko na kujaa lugha chafu za matusi huku wakishindwa kuyajadili yale ya msingi kwa taifa lao
Kutokana na hali hiyo nchi ya Tanzania itaendelea kubaki maskini na vitu kuendelea kupanda bei kila siku huku kipato cha wananchi kuwa duni kwa kukosa watetezi
Alisema kuwa bunge halijafika sehemu nzuri na kuonekana halina tija kwa wananchi wake na hali hiyo linasababisha wananchi kushindwa kupata ukombozi kwa yale wanayoyakusudiwa
Kwa upande wake msanii wa filamu nchini Rose Ndauka alisema kuwa bunge limekuwa si la wastaarabu na matokeo yake wanajadili vitu ambavyo havina tija kwa jamii
Alisema kuwa Tanzania ni nchini ya wastaarabu na wajadili vitu vya ustaarabu kwa kufikia muafaka hali hiyo imekuwa tofauti sasa kwa baadhi ya wabunge kujadili vitu kwa lugha chafu hali inayoshangaza taifa
"Wananchi tumewachagua wabunge huku tukiamini kuwa watafanya hilo tulilowaagiza ila hali imekuwa tofauti na mika mingine baadhi ya wabunge kuanza kujadili vitu visivyo na tija kwa wananchi wao" alisema Ndauka
No comments:
Post a Comment