Wakati
Ikulu ya Marekani ikitangaza kuwa Rais Barack Obama anatarajiwa
kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia Julai Mosi hadi 3,
Serikali ya Tanzania imesema ujio huo utasaidia kuinua uchumi kutokana
na kufaidika na uwekezaji na misaada mbalimbali.
Rais Obama anatarajiwa kuzitembelea Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Taarifa
ya Ikulu ya Marekani iliyotolewa na Ubalozi wa nchi hiyo nchini,
inasema Rais Obama atazuru Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, ikiwa
ni moja ya sehemu ya kuimarika uhusiano baina ya nchi yake na bara la
Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mahadhi Juma alisema ziara ya kiongozi huyo inatarajiwa
kuinufaisha Tanzania maeneo ya biashara na uchumi.
Rais Obama
ambaye ana asili ya Kenya ambako anatoka baba yake mzazi, baada ya
kuchaguliwa kushika madaraka nchini mwaka 2009, alimwalika Rais Kikwete
akiwa kiongozi wa kwanza kwenda Marekani kujadiliana masuala
mbalimbali.
Ziara yake ya kwanza kwa bara la Afrika aliifanya nchini Ghana ambako alihutubia Bunge.
No comments:
Post a Comment