Straight kutoka Bongomovie muigizaji maarufu nchini anae celebrate
freedom yake uraiani kwasasa talk about Kajala amefunguka kuhusu mpango
wake wa kushoot filamu itakayo yaanika maisha yake halisi kutoka kitaa
hadi gerezani.
Kajala ambae hivi kaibuni aliponea chupuchupu
kuhukumiwa kifungo cha
miaka 7 jela kutokana na tuhuma za kushirikiana na mume wake Faraji
Augustino kutumia visivyo fedha za serikali amesema filamu hiyo ina
lengo la kutoa elimu ya namna ya kujiepusha na mazingira yanayoweza
kugharimu muda na maisha ya mtu.
Gonga continue reading kuendelea..
Hata hivyo kufuatia uvumi kuwa Star huyo alichora tattoo yenye jina la
Wema Sepetu mgongoni kwake kama ishara ya kurudisha fadhila kwa shost
yake amekanusha na kusema kuwa kwasasa ni mapema kusema kuwa anaweza
kumlipa wema fadhila isipokuwa tattoo mgongoni kwake ni ishara ya
appreciations kwa rafiki yake.
Muigizaji huyo ambae amemtaja Wema Sepetu kama Hero wake amewataka
mabinti kutokimbilia mali za wanaume bila kujua zinavyopatikana na
badala yake wajishughulishe ili kuepuka hatari ya kungia kwenye mkumbo
utakao yagharimu maisha yao.
Huenda Jumamosi hii ikafanyika ‘Get together party’ Ambasador Launge
maalumu kwa ajili ya Kajala ambapo kila mtu ataingia kwa kiingilio cha
shilingi 10,000 lengo ikiwa ni kuwezesha watu mablimbali kukutana na
msanii huyo asilimia 50% ya fedha zitakazo patikana ikiwa ni halali
yake.
No comments:
Post a Comment