Friday, April 26, 2013

GODBLESS LEMA AKAMATWA....POLISI WAVUNJA MLANGO NA KUMTIA PINGU


Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi wa Polisi wakati wa usiku  wa manane, Mh. Lema alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.


Kukamatwa  kwake  kulikuja  baada  ya polisi  kuvunja mlango na kuingia ndani  na  kuendesha  msako  wa  nguvu  humo  ndani .Vitu  kama laptop, ipad, simu vipo mikononi mwa police. 
Wananchi wengi walijitokeza ku-support mbunge wao na huenda Asubuhi wananchi wakawa wengi zaidi.


Safari ya Lema  kuelekea  polisi  ilisindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza kumsupport kuelekea kituo cha polisi.

Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa ndani.  Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi wa Chadema waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.

Baada ya  kumtupa  ndani,polisi waliwafukuza wafuasi  hao wa Chadema  hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo...
.......

 MH. LEMA AMEKAMATWA KUFUATIA KILE KINACHOTAJWA NA MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUWA YEYE NDO CHANZO CHA VURUGA NA KUZOMEWA KWAE NA WANAFUNZI ALIPOFIKA CHUO CHA UHASIBU NJIRO BAADA YA TUKIO LA KINA MMOJA ALIYEUAWA KWA KUCHOMWA KISU.

KUFUATIA HILI KUNA SINTOFAHAMU NYINGI KWANI ZIMEZAGAA VIDEO CLIPS ZINAZOONYESHA STEPS ZOTE TANGU LEMA AENDE KUTULIZA FUJO CHUONI HAPO HADI MKUU WA MKOA ALIPOFIKA KITU AMBACHO KUTOKANA NA VIDEO HIZI HAPA CHINI WEWE KAMA MFUATILIAJI UNABAKI NA JIBU LAKO.

TAZAMA VIDEO HIZI MBILI KISHA UTAJUA LEMA KACHOCHEA MKUU WA MKOA KUZOMEWA AU KAONEWA........


SISI HATUNA JIBU VIDEO YA KWANZA INAMUONYESHA LEMA AKITULIZA VURUGU ZA WANAFUNZI KABLA MKUU WA MKOA HAJAFIKA 

No comments:

Post a Comment