Thursday, May 9, 2013

2FACE AUZA NGUO ZAKE KUSAIDIA YATIMA


2 face idibia

Mwanamuziki 2face Idibia ameamua kutoa pea ya viatu pamoja na kofia ambayo alivaa katika harusi yake ya kiasili kwa ajili ya kuuzwa ili kupatikana kwa fedha za kusaidia kituo cha watoto ambao wamepoteza mama zao huko Lagos.
Viatu hivi pamoja na kofia zitauzwa kwa njia ya mnada kupitia minada ya hisani ya vitu vya watu maarufu, Kaymu Celebrity Charity Auctions ambayo pia hufanya kazi hii kwa njia ya mtandao.
Mpango huu ulianzishwa mwezi uliopita, na mchango wa 2Face unatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma mbele shughuli za kituo hiki ambacho kinasaidia watoto kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment