Esma
Abdul ambae ni dada yake mwimbaji staa wa Tanzania, Diamond Platnums,
amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae
anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny.
Esma
ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi
yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi
nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye
ataniingilia kwenye mapenzi yangu."
Huu
ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema
nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini
itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa.
Zaidi
ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake
imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia
akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan -
Hyundai IX 35.
Mpaka sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma kama Jokate, Wema Sepetu na wengine.
No comments:
Post a Comment