Umoja wa Mataifa (UN) umeshauri kula wadudu wengi ili kukabiliana na janga la njaa. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo la UN, kula wadudu wengi kunasaidia kuongeza virutubisho mwilini na pia kupunguza uharibifu wa mazingira.
Tayari watu zaidi ya bilioni mbili duniani wanakula wadudu kama sehemu ya mlo wao. Hata hivyo, UN imekubali kuwa bado kuna watu wengi hasa kutoka nchi zilizoendelea ambao wanaona kinyaa kula wadudu.
UN imesema kuwa kwa sasa wadudu kama manyigu na kombamwiko wanatumika kwa uchache sana kama sehemu ya mlo. Ripoti hiyo imesema kuwa wadudu wapo kila sehemu na wanazaliana kwa wingi sana lakini hawatumiki kama chakula.
Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa wadudu wana virutubisho, hasa protini, mafuta na madini. Wanadai wadudu ni muhimu sana kama chakula hasa kwa watoto ambao hawapati lishe ya kutosha.
Ripoti hiyo imeshauri kuwa sekta ya chakula inaweza kusaidia kwenye kampeni ya kula wadudu kwa kujumuisha recipes mpya za wadudu katika vyakula vyao na kuongeza wadudu kama menu kwenye mahoteli.
Uko tayari kula wadudu kama kombamwiko (mdudu wa jamii ya memde) kama sehemu ya mlo wako?
No comments:
Post a Comment