Rapper
Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema mara nyingi wasanii wakongwe
huishia kulalamika wanapochuja kwakuwa hushindwa kubadilika kuendana na
wakati na pia kupenda kuchukuliwa kama ‘malegendary’ hata kama wakichemka kwenye kazi zao mpya.Ameongeza kuwa mara nyingi wasanii wengi hufika hatua ya kuanza kulalamika kwakuwa muziki wa Tanzania hauna mipango inayoeleweka.
“Hivi
vitu vingi vinaletwa kwasababu muziki wetu hauna mipango,industry
yetu ipo very disorganized. Kwasababu hiyo inafanya watu wamekuwa
wakubwa na wamekaa muda mrefu kwenye muziki na nguvu zinaanza
kuwapungua wakati hawajafikia yale malengo na wanajiona hawana
chochote,”amesema FA.
“Hii
inaleta matatizo kidogo. Sitaki kusema vibaya, kiLa mtu ana madai yake
pengine na mimi siku moja nitakuja kulalamika, you understand, lakini
nachosema ni kwamba nafikiri watu wawe reasonable tuangalie hivi vitu
kama biashara, tusiangalie vitu kwa ubinafsi it’s never personal you
know,” ameongeza FA.
“Jivishe viatu vya mtu ambaye unamlalamika labda,
kama wewe ungekuwa na nafasi yake, na yeye yupo katika nafasi yako
ungemtreat vipi nakadhalika. Tusijipe ile superiority complex kwamba
mimi ni Mwana FA kwahiyo natakiwa nikitoa wimbo
wangu upigwe kwa hali yoyote, mimi ni AY nikitoa wimbo wangu lazima upigwe kwa hali yoyote ile hata kama nimechemka ama nini.
Tufike
mahali tuangalie tushindane na soko kila mtu anafanya muziki wake
Mwana FA ni Mwana FA hawezi kushinda na Godzilla hawezi kushindana na
Nikki Zohan. Lakini natakiwa nitengeneze class ya Mwana FA niangalie
angle ambayo ninatoka, kama siku zote ambavyo tumekuwa tunafanya.
Tuangalie kwamba soko limebadilika na inabidi tuende nalo kwa kasi hiyo
hiyo badala yake tukitaka kuwa treated kama malegendary tutaishia
kulaumu watu tu.”
No comments:
Post a Comment