Monday, May 20, 2013

Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM) ataka JamiiForums IFUNGIWE NA SERIKALI



Akiwa katika kipindi cha Jambo kikirushwa toka Bungeni akiwa na Mbunge wa Kasulu bwana Machari.

Mh. Machali kausifia mtandao wa JF kuwa unapendwa na chanzo kizuri cha habari kwa Jamii hasa Tanzania na kama mkombozi kwa habari

Cha kusikitisha sana Bwana Alhaj Juma Nkamia Kadai ni mtandao ambao hauna sifa ya kuitwa mtandao wa kijamii kwani unaandika uwongo na mambo ya kufikirika na utashi wa mtu

Anadai anajua lazima tumwandike na hataacha kusema. Anadai kuwa serikali inadai kuwa haiwafahamu wanaoandika utumbo katika mitandao kama jamii forum lakini anahoji iweje kama jamii forum kuna matangazo ya biashara na ni wazi kuwa wamiliki wake wanafaamika kwanini hawachukuliwi hatua?

No comments:

Post a Comment