Baba Askofu Mstaafu Norbert Mtega, akijibu maswali ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma.
Picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi hao.(Picha na Juma Nyumayo)
---------------------------------------------------------
Na Nathan Mtega,Songea
SIKU
moja baada ya Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbet
kutangaza kustaafu nafasi hiyo kauli ambayo ilizua maswali na mijadala
mingi miongoni mwa waumini wa kanisaa katoliki nchini na wananchi kwa
ujumla ameamua kuzungumza na waandishi wa habari mjini Songea kufafanua
zaidi kuhusiana na uamuzi wake huo.
Alisema
kuwa ni wazi kuwa uamuzi huo aliouchukua umewashitua wengi lakini
amelazimika kufikia uamuzi huo kufuatia kukumbwa na matatizo ya kiafya
yaliyojitokeza kwake katika siku za hivi karibuni ambayo hakuwahi
kuyapata kwa miaka mingi ya maisha yake pamoja na utume.
Askofu
Mtega aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye ataendelea kuitwa Askofu
mkuu mstaafu na amepanga kuendelea kuishi ndani ya jimbo kuu la
Songea na yuko tayari kueendelea kutoa ushurikiano kwa kiongozi
mwingine atakaeteuliwa kushika nafasi hiyo huku akiiasa jamii kuishi kwa
amani na utulivu na kuepuka kubaguana kwa misingi ya dini,ukabila na
itikadi za kisiasa bali waweke moyo wa uzalendo wa taifa mbele.endelea kupitia na kukopi audifacejackson blog.Alisema
kuwa ameona ni vyema akakaa pembeni ili aweze kupata muda mzuri wa
kupumzika na kupata matibabu ili afya yake ikitengamaa aweze kuwa
mashauri mzuri kuliko kuendelea kunga’ang’ania mpaka afikike hatua ya
kupoteza kumbu kumbu na kuwa kikwazo na hoja ya jimbo kuzorota katika
siku za mbele.
Akijibu
maswali ya baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na mambo ambayo
angependa ayaone yakifanyika alisema kuwa suala la elimu nchini siyo la
kulipuuza na linapaswa kuwekewa misingi mizuri na imara kuanzia ngazi ya
elimu ya msingi kwa sababu utaratibu uliopo wa kufanyia marekebisho
alama za wahitimu waliofeli katika mitihani haulisaidii taifa kielimu
pamoja na uhifadhi wa mazingira ambayo yanaendelea kuharibiwa kwa kasi
kubwa na jukumu la kuvinusuru hivyo vyote ni la kila mmoja kwa maslahi
ya taifa.
Aidha
aliwataka viongozi wa kanisa katoliki jimboni humo kujikita zaidi
katika kuimarisha imani kwa waumini katika kanisa hilo ambalo yeye
amelitumikia kwa kipindi cha miaka 22 na Jimbo la Iringa ambalo
alilitumikia kwa kipindi cha miaka sita ambalo kwa sasa linaongozwa na
Askofu Tarciusi Ngalalemkutwa ambaye sasa ataliongoza pia jimbo kuu hilo
la Songea linaloachwa na Askofu Mtega.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment