Irene Uwoya.
MASTAA
wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya na Blandina Chagula ‘Johari’
wametimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwenda kurekodi filamu. Akizungumza
na paparazi wetu hivi karibuni kwa njia ya simu akiwa nchini humo,
Uwoya alisema wamekwenda nchini humo kurekodi sinema ambayo Watanzania
wataitambua ikikamilika. Pia wataunganisha na ziara ndefu katika nchi
mbalimbali barani Afrika zikiwemo Namibia, Ghana, Lesotho na kwingineko
kujifunza soko la filamu.
Blandina Chagula ‘Johari’.
“Tupo
huku na Johari lakini tutakuwa na ziara ndefu sana ya nchi mbalimbali
za Afrika kwa ajili ya kulisogeza soko letu la filamu na kujifunza
jinsi wenzetu wanavyofanya katika filamu zao,” alisema Uwoya.
No comments:
Post a Comment