KATIKA
hali isiyo ya kawaida, ugomvi mkubwa umetokea kwenye Kanisa la AICT, kati ya
baadhi ya wanakwaya wa kanisa hilo linalofahamika kwa jina la “Bupandwa” na
mchungaji wao Petro Masule.
Tukio hilo la aina yake, limetokea kwenye Kijiji Bupandwa,Kata ya
Bupandwa, Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza.
Wanakwaya hao walisimamishwa kutoa huduma Kanisani kwa
njia ya uimbaji kwa kosa la utovu wa nidhamu ambapo ugomvi huo, ulitokea Mei 12
mwaka huu, baada ya ibada.
Inadaiwakuwa , Mchungaji Masule
hakutumia lugha nzuri baadayakuwaitawanakwaya hao “watenda dhambi ambao
hawapaswi kuingia katika hekalu la Bwana”.
Kauli hiyo inadaiwa kuwakera
wanakwaya hao ambao kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo, walisema Mchungaji
Masule aliyasema hayo katika mahubiri ya ibada ya kwanza.
Mchungaji huyo alidai kuwa, kutokana
na makosa waliyotenda wanakwaya hao, wanapaswa kutubu ili waweze kuingia
kanisani.
Baada ya ibada hiyo kumalizika,
baadhi ya wanakwaya waliokuwa wamesimamishwa ambao walihudhuria misa hiyo,
waliamua kuungana na kumfuata Mchungaji huyo akiwa na wazee wa kanisa
wakihesabu sadaka.
Wanakwayahao walimuomba Mchungaji
huyo awape vyombo vya kuimbia ambavyo walidai kuvinunua kwa fedha zao ili
wakaazishe kanisa lao wakidai kukerwa na mahubiri yake.
Kutokana na matakwa ya wanakwaya
hao, ilitokea vurugu kubwa ndani ya kanisa hilo kati yao na Mchungaji Masule,
ambapo katika ugomvu huo, inadaiwa muumini mmoja aliumia sehemu mbalimbali za
mwili wake.
Gazeti hili lilipomtafuta Mchungaji
Masule, alikiri kuzipiga na wanakwaya ndani ya kanisa hilo ambao walikiuka
maadili na matakwa ya kanisa kwa kutokufuata sheria na kanuni.
Kwa
upande wake, Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Vincent Ngidingi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, kulaani kitendo kilichotokea kanisani hapo na kuwaasa
waumini kufuata sheria za kanisa.
No comments:
Post a Comment