JESHI
la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia baadhi ya wanenguaji wa
kundi maarufu kwa kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si
Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo lina hatimiliki ya hii habari.
Watuhumiwa
hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza
miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambamba na watu
hao walikamatwa katika maeneo ya Hoteli ya Travertine, Ambiance Club,
Kinondoni Makaburini, endelea kupitia na kukopi audifacejackson blog.Coco Beach na Barabara ya Tunisia.“Tumewakamata
hao wanaofanya mchezo maarufu wa Kangamoko na Laki si Pesa na tayari
wanafikishwa mahakamani muda wowote na msako bado unaendelea ili
kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au baikoko ambayo
watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.
Kundi
la kangamoko limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara kutokana na kucheza
wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia
maji.
Kukamatwa
wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katika
Bunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwa wakipotosha jamnii.
No comments:
Post a Comment