Msichana
mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa
dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland
na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.
Tintswalo
Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo
la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta
hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha
yake ya anasa.
Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.
Tintswalo,
ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu
wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba
la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema
'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.
"Wake
zake wamewekwa kwenye majumba yao, wakizingirwa na walinzi, na hakika
hawawezi kwenda kokote isipokuwa tu mfalme akisema hivyo. Kitu pekee
wanachofanya ni kwenda Marekani mara moja kwa mwaka, wakati mfalme huyo
anapowapatia posho kwa ajili ya manunuzi."
Tintswalo
alikuwa amelazimishwa kuachana na maisha ya starehe kwenye shule moja
ya bweni huku shangazi yake, ambaye alikuwa mlezi wake mkuu, akisuka
mipango ya kutorokea Uingereza kuungana na mama yake, ambaye alihamia
mjini Birmingham miaka mitano kabla, akimtoroka mume wake mnyanyasaji.
"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka tu."
Tangu
kuwasili nchini Uingereza, Tintswalo amekuwa sauti ya upinzani dhidi ya
utawala kandamizi za Swazi, ambapo vyama vya upinzani vya siasa
vimefungiwa na wanaharakati wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara au
kushambuliwa.
Hatahivyo,
shughuli kuu za Tintswalo, ikiwamo maandamano ya kila wiki nje ya
ubalozi wa Swazi mjini London akiwa na kikundi cha Swazi Vigil,
zimesikika kwa mamlaka hizo nchini kwake na sasa anaamini yuko kwenye
hatari kubwa zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.
Alisema: "Hivi
karibuni nilipata taarifa kwamba watu wametumwa kutoka Swaziland kuja
kunikamata, jambo ambalo hakika linanitisha mno. Kama nikirejea,
nitakamatwa au mbaya zaidi huku pale kuna watu ambao wanateseka, kupigwa
au kuuawa kwa kujihusisha na siasa."
Tintswalo
sasa anaishi katika mashaka ya kuweza kurejea nchini Swaziland, baada
ya ombi lake la kwanza la hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza mwaka 2007
kukataliwa mwaka 2011.
Mwezi
uliopita, alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha kushikilia wahamiaji
baada ya miezi 18 ya kuripoti kila wiki katika mamlaka hizo.
Hatahivyo,
baada ya shinikizo kutoka TUC na ofisi ya Mbunge wa Birmingham kupitia
chama cha Labour, Roger Godsiff, Tintswalo aliachiwa na sasa amekata
rufaa wizara ya Mambo ya Ndani.
Godsiff alisema juzi: "Tumefurahishwa mno wanasheria walifanikiwa sana katika kuwezesha kutazamwa upya kwa kesi ya Ngobeni."
Baba
huyo wa watoto 27, Mfalme Mswati III alikuwa mgeni kwenye harusi ya
William na Kate na pia kwenye sherehe za Miaka 50 ya Malkia wakati wa
majira ya joto mwaka jana.
Mke
wa sita wa mfalme huyo alitoroka kutoka kwenye jumba hilo harimu mwaka
jana, akielezea miaka kadhaa ya 'machungu na udhalilishaji wa kimwili'
uliofanywa na mume wake.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani alikataa kuzungumzia chochote.
No comments:
Post a Comment