Wednesday, May 22, 2013

WASTARA RUKSA....... KUOLEWA


Wastara Juma.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika kilicho karibu na msanii huyo, zinasema kwamba Wastara amemaliza salama eda yake baada ya kufiwa na mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari, mwaka huu.
Staa huyo bado yupo Muscat, Oman alikoitwa na ndugu zake kwa ajili ya kukaa eda hiyo na kupumzika baada ya kupata masaibu ya kuondokewa na mumewe kipenzi.
KAMA MWARABU
Chanzo kinaeleza kuwa uamuzi wa Wastara kwenda kukaa eda Uarabuni ni mzuri kwa sababu kwa sasa yupo vizuri kiafya na mawazo ya kuondokewa na mwenzake yamepungua.
“Ni kweli kifo hakizoeleki lakini Wastara amejitahidi sana kutuliza kichwa chake. Ndugu zake wamemsaidia sana, wamekuwa naye katika kipindi hiki kwa upendo wa hali ya juu.


“Yaani ukimuona jinsi alivyopendeza utashangaa, ni kama Mwarabu kabisa. Mungu mkubwa sana jamani, kila mtu anafurahishwa na jambo hilo. Mungu ataendelea kumsimamia,” kilipasha chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake gazetini.


Wastara akiwa Uarabuni.
KUTUA BONGO
“Kwa sasa anaendelea kupumzika kidogo, mwezi ujao (akimaanisha Juni) tarehe za mwanzoni kabisa atarudi Dar.
“Kitu kikubwa anachowaza kwa sasa ni kurudi tena na kusimama kwenye kazi ya uigizaji ili aweze kulea familia yake, maana yupo peke yake.”


HUYU HAPA WASTARA


Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kuzungumza na Wastara kwa njia ya simu ambaye alithibitisha kumaliza eda yake na kwamba atarejea Bongo mwezi ujao.
...Wastara katika pozi.
“Namshukuru sana Mungu wangu, nawashukuru pia ndugu zangu kwa moyo wao wa upendo na kunijali katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mume wangu. Naendelea vizuri na mwezi ujao nitarudi huko nyumbani,” alisema.


Alipoulizwa kuhusu suala la ndoa mpya baada ya eda yake, alisema: “Nimewahi kujibu swali la namna hii. Kiukweli sifikirii chochote kuhusu suala la ndoa. Nahitaji kutuliza kichwa changu.”NA GLOBAL PUBLISHER

No comments:

Post a Comment