Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach.
Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesemawanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.
Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu.
Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa
No comments:
Post a Comment