Diamond akiwa katika pozi na mpenzi wake Penny.
MSANII anayekimbiza katika anga za Muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' leo amefunguka kuwa hana tena mapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, mrembo Wema Isaack Sepetu.
Akihojiwa na Zamaradi Mketema katika kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, Diamond ameeleza anavyomfeel sana mpenzi wake wa sasa Penny ambaye anadai anamuheshimu na wala hamcheat. Kuhusu kutoka kimapenzi na wasanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya pamoja na Aunt Ezekiel, Diamond ameruka kwa kusema kuwa anamheshimu sana Uwoya wakati akidai kuwa Aunt alikuwa demu wa mshikaji wake. Mkali huyo ameweka wazi pia kuhusu mapenzi yake na Jokate kwa kummwagia sifa kadhaa na kueleza kuwa yeye ndiye mwenye makosa maana Jokate alikuwa innocent na hakuwahi kumkosea japo aliachana naye na kurudi kwa Wema kabla hajaangukia kwa mrembo Penny ambaye ndiye anataraji awe mama watoto wake.
No comments:
Post a Comment