Monday, May 20, 2013

ASKARI MAGEREZA MWENYE CHEO CHA KOPLO ANUSURIKA KIPIGO BAADA YA KUDAIWA KULAWITI VIJANA MOROGORO. by Jackson Audiface


Askari wa jeshi la magereza wakionyesha uhidari wao katika gwaride, picha hii ni ya maktaba haiusiane na tukio hili.
ASKARI magereza mwenye cheo cha Koplo amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kubainika kuwalawiti kwa siku moja vijana wawili wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 20.
Tukio la kuwalawiti vijana hao linadaiwa kufanywa na askari huyo kati ya majira ya saa 7.00 mchana  na saa 2.00 usiku katika moja ya nyumba za kulala wageni (jina limehifadhiwa) iliyoko mtaa wa Mafisa manispaa ya Morogoro.
Akisimulia mkasa huo, Meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni jina tunalo alisema kuwa imekuwa ni desturi ya askari huyo kwenda na vijana wa kiume katika nyumb

Alisema kuwa siku ya tukio askari magereza huyo alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni majira ya saa 7.00 mchana akiwa amempakia kijana mmoja katika pikipiki yake na kabla ya kukabidhiwa funguo ya chumba namba 202, mhudumu wa nyumba hiyo alimwambia askari magereza huyo kuwa masharti ya nyumba yao hayaruhusu watu wa jinsia mmoja kukaa chumba kimoja.


Alisema kuwa askari huyo alimtambulisha kijana aliyekwenda naye pale kuwa ni mdogo wake na kwamba walikuwa na mazungumzo naye ya muhimu na baada ya mazungumzo hayo kijana huyo angeweza kuondoka.


Hata hivyo, muda mfupi baada ya watu hao kuingia chumbani mmoja wa wahudumu alipita karibu na mlango wa chumba hicho na kusikia sauti ya mahaba, hali iliyomtiwa wasiwasi na kulazimika kuripoti tukio hilo kwa meneja wake.


Majira ya saa 11.00 jioni askari huyo alitoka na kijana huyo na kuahidi kurudi tena baadaye na aliporudi majira ya saa 1.00 usiku alirudi na kijana mwingine anayedaiwa kuwa mwenyeji wa mkoa wa Tanga na kwa siku hiyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam baada ya kupigiwa simu na askari huyo.


Askari huyo alingia chumbani akiwa na kijana huyo na muda mfupi alitoka na kwenda dukani kununua kodomu na mafuta ya mgando pasipokujua kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wakifuatilia nyendo zake.


Aliporudi na kuingia chumbani baadhi ya vijana waliokuwa wameandaliwa walizunguka nyuma ya chumba hicho na kuchungulia dirishani na ndipo walipojionea mambo yote yaliyokuwa yakiendelea chumbani humo.


Majira ya saa 2.00 usiku baada ya mambo hayo kumalizika kijana huyo alitoka na kumuacha askari huyo akioga hata hivyo kabla hajafika mbali meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa na wakazi wengine wa mtaa huo walionesha kukerwa na kitendo kile walimvamia kijana huyo wakitaka kumhoji sababu za kushiriki kitendo kile cha aibu.


Hatahivyo, wakati wananchi hao chini ya mjumbe wa seriakli ya mtaa wa Mafisa, Amina Mandawa,  wakiendelea kumbana kijana huyo askari huyo alifika katika eneo hilo akiwa na pikipiki yake na kujikuta akipokea kipigo baada ya kubainika kuwa ndiye aliyekuwa akimlawiti mtoto huyo.


Kufuatia dhahama hiyo, askari polisi wanaotumia pikipiki maarufu kama ‘Vodafasta’ alifika katika eneo hilo na kuwanusuru watu hao na kibano cha wananchi na kufanikiwa kuwapeleka kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano.


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, amekiri jeshi lake kumshikiria askari magereza pamoja na kijana anayedaiwa kulawitiwa na askari huyo kwa muda kabla ya kuachiwa kwa dhamana siku hiyohiyo majira ya saa 8.00 usiku.


Kamanda Shilogile alisema kuwa tayari jalada limefunguliwa na kupelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali kama ilivyo utaratibu wa sasa ambapo kesi zote za jinai hazisimamiwi na jeshi hilo kama ilivyokuwa awali.


Habari zaidi zinadai kuwa askari magereza huyo amehamia mkoani Morogoro miezi minne iliyopita akitokea Arusha ambako nako inadaiwa alihamishwa kutokana na kuwa na tabia ya kulawiti vijana wadogo. 
IMENADLIWA NA: 
Venance George, Hamida Shariff na Juma Mtanda, Morogoro

No comments:

Post a Comment