MWENYEKITI WA CCM DK JAKAYA KIKWETE.
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amefungua milango kwa
kuwataka baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowania urais mwaka
2015 kuendelea na mchakato huo.
Rais
Kikwete amewatahadharisha watu hao kuendesha kampeni zao kwa ustaarabu
pasipo kuibua chuki wala kujenga makundi ambayo alisema ni hatari kwa
kuwa yanaweza kukipasua chama.
Rais
Kikwete aliyasema hayo katika mkutano ndani wa wabunge wa chama hicho
uliofanyika jana katika ukumbi wa CCM (white house) mkoani hapa.
Mkutano
huo ambao ulianza saa 3.00 asubuhi ulilenga kujadili masuala mbalimbali
ya taifa ikiwamo utekelezaki wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho katika
majimbo na ahadi mbalimbali za viongozi wa taifa.
Chanzo
chetu cha habari kutoka ndani ya ukumbi huo kilieleza kuwa Rais Kikwete
aliwataka wanachama wenye nia ya kugombea urais kuwa na tahadhari na
watu aliowaita vishoka wa siasa.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete alisema watu wa aina hiyo wana tabia ya kula huku na h
uku kwa kujiingiza katika kambi zaidi ya moja.
“Tuangalie
makundi ya urais 2015 yasishambuliane kwa kuvunja chama, wenye nia hiyo
ya kugombea waendelee na mikakati yao kujenga chuki kwa makundi
mengine.
“Katika
hatua hiyo, pia mkumbuke kuwa katika kambi hizo za urais zinatakiwa
kujitizama wao na wafuasi wao maana wafuasi wengine hawaaminiki, ”
alisema Rais Kikwete.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa ajenda alizokuwa nazo Rais Kikwete
ni pamoja na suala la urais na utendaji wa wabunge majimboni.
Rais
Kikwete aliwataka wabunge wa chama hicho kubadili mwenendo wa
kuyatelekeza majimbo yao na badala yake akawahimiza kujenga tabia ya
kutembelea majimbo yao mara kwa mara.
“Hili
JK amelisemea kwa ukali kwamba tabia ya baadhi ya wabunge kuhamia
mijini na kutelekeza majimbo yao ni hatari kwani mwisho wa siku wananchi
watawanyima kura na kuzipeleka upinzani.
“Pia
alikemea tabia ya baadhi ya wabunge kununa na kuwachukia watu wengine
wenye nia ya kugombea katika majimbo yao. Akasema mbunge asiyetimiza
wajibu wake kwa wananchi wake na bungeni ni vigumu kubaki.
“Wanatakiwa
kurudi majimboni kwao kusimamia ilani ya chama pamoja na ahadi zao
walizoahidi na zile za viongozi wa chama na Serikali ikiwamo ahadi zake
kama rais,” alisema.
Kuhusu
suala la ukosoaji, Rais Kikwete alisema wabunge wa chama hicho wana
wajibu wa kuikosoa Serikali yao lakini akaonya aina ya ukosoaji wenye
lengo la kuibomoa Serikali.
“Mnatakiwa
kuisimamia Serikali na kuikosoa bila kuibomoa, lakini kuna baadhi yenu
mmekuwa mkiibomoa Serikali kwa jinsi mnavyochangia huko bungeni… hilo si
jambo jema hata kidogo, waachieni wale wenzetu,”alisema Kikwete.
Chanzo
hicho kilieleza kuwa wabunge wamekuwa hawaridhishwi na utendaji wa
baadhi ya mawaziri ambao walisema ni mizigo na kutaka waondolewe katika
nafasi zao.
Chanzo
hicho kilitaja majina ya mawaziri hao wanaodaiwa kuwa ni mizigo kuwa ni
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. David David Mathayo, Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenera Mkangara.
Baadhi
ya wabunge walimtaka Rais Kikwete kudhibiti ubadhirifu unaofanywa na
baadhi ya watendaji wa halmashauri mbalimbali nchini, wakuu wa wilaya na
wakuu wa mikoa.
“Rais anatakiwa kukunjua makucha yake kuondokana na uozo huu katika halmashauri zetu.
Haiwezekani
waendelee kunyamaziwa, tunatakiwa kuimarisha chama kwa kuangalia namna
Serikali inavyoweza kutimiza ahadi kwa wananchi,” kilisema.
Kiliendelea
kusema. “Serikali iweze kusaidia katika kutimiza ahadi kwa kutelekeza
ilani ya chama, viongozi wa vijiji, kata na vitongoji kuanza kulipwa
mshahara maana wamejitolea kwa muda mrefu hivyo huwalazimu kupata
ushawishi kutokana na njaa,” kilisema.
Imeelezwa kuwa katika kikao hicho kinachoendelea kitakuwa na ajenda nyingi ambazo zitaibuliwa na wabunge.
Hizo ni pamoja na maslahi ya wabunge, utendaji kwa baadi ya mawaziri na aina ya ukosoaji inayofanywa na
No comments:
Post a Comment