Wanafunzi
wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya
biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi stadi [VETA],Dar
es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya
biashara ya kuuza mili yao.
Washitakiwa hao
waliokamatwa katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni
ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na
wote walifikishwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilikuwa
chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John
Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira
tofautitofauti.
Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye
miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa
kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.
“Nilikwenda
pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita
nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija
akijitetea.
Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa hao
wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa
na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.
Wakati
huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716
waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38
na wanawake 678.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema
watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo
mbalimbali ya Kinondoni.
Maeneo hayo ni baa, kumbi za
starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na
makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja
na wateja wa machagudoa.
“Msako huo ulifanyika Maisha
Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja
wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema
Kamanda
Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka
nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka
huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.
Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.
Chanzo Majira....
No comments:
Post a Comment