Monday, May 20, 2013

TANGAZO KUTOKA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUHUSU KUFUNGULIWA CHUO


CHUO CHA UHASIBU ARUSHA
TAARIFA YA KUFUNGUA CHUO
Chuo cha Uhasibu Arusha kinawatangazia Wanafunzi wote wa kozi 
za ngazi ya Cheti hadi Stashahada ya Uzamili kwamba chuo 
kitafunguliwa siku ya Alhamisi tarehe 23 Mei, 2013.
Kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 27 Mei, 2013 kutakuwa na zoezi la 
usajili katika lango kuu la kuingia chuoni kwa kuzingatia masharti
yafuatayo:
1. Kila Mwanafunzi aliyeomba upya kujiunga na chuo anapaswa 
kuonyesha kitambulisho chake cha chuo.
2. Kila Mwanafunzi aje na risiti au “Bank pay in slip” ya 
kuonyesha malipo ya karo na fedha zote anazodaiwa na chuo.
3. Kila Mwanafunzi anapaswa kuingia mkataba mpya na Chuo. 
Mkataba huo unapaswa kusainiwa kabla Mwanafunzi 
hajasajiliwa.
4. ANGALIZO: Hakutakuwepo na usajili baada ya tarehe 27 Mei,
2013.
Mkuu wa Chuo

No comments:

Post a Comment