Friday, May 24, 2013

DIAMOND ATIA AIBU YA MWAKA....KINGERZA CHAMUUMBUA TENA


KWANZA  NAANZA  KWA  KUMPONGEZA  SANA  DIAMOND maana  akiwa hajamaliza hata wiki mbili tangu atoke kwenye tour iliyofanikiwa ya Burundi na Congo, Diamond leo amesaini mkataba wa show nyingine kubwa ya kimataifa.

Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha inayomuonesha akisaini mkataba wa show huku pembeni akiwepo mtu mwenye asili ya Asia ambaye huenda ndio promoter. 

Kilichowafanya  mashabiki wake  huko instagram  wavunjike  mbavu  ni Kingereza  alichotumia.....

"After I DONE did the Uk,Congo,Burundi…guess where next I’ll be headed.”...

Haijalishi  umekosea au upo  sahihi, ujumbe  umefika  kaka!!.  Waache  wacheke, wataacha  tu.

 Hata  hivyo, si vibaya pia  kutumia  lugha  yetu ya kiswahili  maana  ujumbe  hufika  vizuri  zaidi....Kingereza lugha ya  watu...ni ngumu..!!! 

No comments:

Post a Comment