Wednesday, May 22, 2013

HUYU NDIYE MKENYA ALIYECHINJA WATU 400 KWA PANGA APEWA HIFADHI UINGEREZA.


John Thuo.
Muuaji ambaye aliua karibu watu 400 nchini mwake amepatiwa hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza.

John Thuo, mwenye umri wa miaka 27, ambaye aliwacharanga wengi wa waathirika wake katika mashambulio ya kutumia mapanga nchini kwake Kenya, ametumia takribani miaka 10 akiishi nchini Uingereza kwenye makazi ya bure iliyotolewa na Huduma ya Taifa Kusaidia Hifadhi ya Kisiasa.
Anaaminika kupokea marupurupu yanayofikia Pauni za Uingereza 160 kwa mwezi kutoka huduma hiyo, kitengo cha Wizara ya Mambo ya Ndani kinachoshughulikia makazi kwa wanaotaka hifadhi ya kisiasa.
Thuo, ambaye alikuwa mfuasi wa kundi halifu la Mungiki nchini Kenya, alikiri mbele ya mahakama ya uhamiaji kwamba aliwaua 'takribani watu 100 hadi 400'.


Pia alishiriki katika kuharibu viungo vya uzazi vya wanawake.
Alipatiwa ruhusa ya kubaki nchini Uingereza kwa miaka mitatu baada ya rufani, chini ya Sheria ya Haki za Binadamu, katika Mahakama ya Uhamiaji na Hifadhi ya Kisiasa.
Anasema kumtimua kutakiuka haki yake ya kibinadamu sababu atakabiliwa na adhabu ya kifo kutoka kwa kundi hilo mara atakaporejea.
Alipofuatwa nyumbani kwake katika mji mdogo wa Coventry, ambako majirani zake hawafahamu chochote kuhusu historia yake ya kutisha, alisema: "Ni kweli - niliua watu wengi. Sipendi kuzungumzia historia yangu iliyopita. Najihisi mwenye hatia kwa nilichofanya. Najihisi kujuta."
Thuo, ambaye amejibana kama mtu aliyeondoshwa katika Uingereza, alisema: "Nimeanza maisha mapya hapa na natafuta kazi za mara kwa mara. Kama nikirejea, watanikata kichwa."
Alipoulizwa kama anafuatiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, alisema: "Hapana, sitakiwi kukutana na yeyote. Niko huru."
Mmoja wa majirani zake kwenye mji huo wa West Midlands alisema: "Sikuwa nikifahamu kuhusu yeye kuua watu wote hao. Inatisha. Kuna watoto wengi wanaoishi katika mtaa huu."
Jirani huyo aliongeza: "Ni mlevi mkubwa mno. Anaweza kununua chupa za pombe aina ya vodka na kunywa. Anapofanya hivyo kubadilika na kuwa mgomvi."
Rufani ya Thuo dhidi ya kuondoshwa Uingereza ilitolewa Machi baada ya shahidi wa kigeni kuthibitisha kwamba wafuasi wa Mungiki wanafahamika kwa kuwakata vichwa wote waliojiengua kutoka kundi hilo.
Jaji huyo pia alizingatia afya ya kiakili ya Thuo, na vitisho kwamba atajiua mwenyewe kama angerudishwa kwao.
Baada ya miaka yake mitatu kwisha, atalazimika kuomba kuongezewa muda au kurejeshwa kwao. Thuo aliieleza mahakama hiyo mjini London alijiunga na Mungiki mjini Nairobi wakati alipokuwa na umri wa miaka 10 tu, lakini alipanda vyeo haraka na kuwa kiongozi wa juu anayeongoza zahama za ulinzi.
Mwaka 2002 alishiriki katika shambulio la kulipiza kisasi kwa wanakijiji ambao walikuwa wamewaua wafuasi wawili wa kundi hilo. Aliwakatakata wananchi wawili kwa kutumia panga. Katika tukio jingine, aliwaua maofisa wawili wa polisi.
Kundi hilo la Mungiki lilipigwa marufuku nchini Kenya mwaka 2002, na Thuo aliwasili nchini Uingereza kama mhamiaji haramu Agosti, 2003.
Alificha utambulisho wake hadi alipohitaji msaada wa Bima ya Afya kutokana na matatizo ya kiakili.
Paul Flynn, Mbunge wa Newport kwa chama cha Labour, alisema: "Inatisha mno kwamba mtu fulani ambaye amekiri kuua watu wengi hachunguzwi na polisi katika nchi yake.
Na pengine inatisha zaidi anaweza anadai na kufanikiwa kupatia hifadhi ya kisiasa licha ya anayosema ameyafanya."
Msemaji wa Aegis Trust, ambayo inaendesha kampeni kuzuia uhalifu dhidi tya ubinadamu, alisema: "Yeyote anayeshukiwa kwa uhalifu wa kimataifa anatakiwa kushikiliwa kwa mashitaka."

Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema: "Tumesikitishwa na uamuzi wa mahakama, lakini tunaweza tu kukata rufani pale kosa fulani la kisheria linapobainika katika hukumu. Katika kesi hii hakukuwa na mwanya wa kukata rufani."

1 comment:

  1. The Casino in St. Louis: What's next for St. Louis?
    Casino in St. Louis is about 태백 출장샵 a 15-minute 김천 출장샵 drive from Louis, Mohegan Sun and 1-mile-long walk from 당진 출장샵 the Convention Center. The hotel is 용인 출장마사지 open 안양 출장샵 24 hours

    ReplyDelete