Dkt Slaa akiwa na mchumba wake Bi Bi.Josephine Mushumbusi Kushoto
Na Esther Macha, Mbeya
Na Esther Macha, Mbeya
UMOJA
wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia
Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Hatua hiyo inatokana na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa
mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri Rais ambaye ni mume wake kuiongoza nchi vizuri .

Kauli
hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya
Bi.Priscilla Mbwaga wakati akitoa Tamko kwa waandishi wa habari juu
ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi kwa Mke wa Rais katika
mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya
Vwawa Mkoani hapa.
Bi.Mbwaga alisema kuwa katika mikutano yake ya Hadhara Bi.Mushumbusi alidai kuwa mama Salma Kikwete ameshindwa kumshauri mume wake kuingoza nchi na kuacha Twiga wakiwa wanakunjwa na kuondoka na kwamba yeye akiwa Ikulu hataacha kumshauri mume wake Dkt.Slaa katika masuala
ya kuingoza Nchi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kama umoja huo wanalaani vikali lugha chafu na za kichochezi zinazopandikizwa chuki miongoni mwa jamii ya watanzania .
Alisema kuwa kama umoja wa wanawake wanalaani matusi hayo na kwamba umoja huo ulifuatilia mikutano hiyo na kugundua kuwa ilikuwa imetawaliwa na matusi badala ya kutoa sera kwa wananchi kuwa wanataka kufanya nini.
“Sisi kama umoja wa wanawake Mkoa tunaeleza umma ambao una imani na kuwa katika utamaduni na maadili yao hawapendi na wala hawajazoea kusikia matusi katika jamii yao hivyo wakiangalie vizuri na kwa makini Chadema kuwa cha hicho kina watu wa maadili gani , mahali pote siku zote na miaka yote ni matusi,kuongea uongo, uzushi na kashfa wasimamapo majukwaani “alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Bi.Mbwaga alisema kuwa wanawake wa mkoa wa Mbeya wanadhani kuwa kauli ambazo zimetolewa na Mushumbusi ni ni za kuwadhalilisha wanawake wote wa Tanzania kwani Mama Salma ni Kiongozi wa juu pamoja
na Mushumbusi .
“Tunamshangaa sana Mushumnbusi anaposimama majukwaani na kutoa kashfa nzito za namna hii ni kama nani kwa wanawake wa Tanzania alihoji Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa (CCM),Bw.Amani Kajuna alisema kauli aliyotoa Dkt.slaa kuwa Rais Kikwete ana Udini ni ulaghai mkubwa ambao anaufanya kwa wananchi na kuendelea kuiweka nchi katika mazingira magumu .
“Kama vijana tunatambua kuwa Rais Kikwete ni kiongozi wa watanzania, na kwamba hana sifa ya Udini hii ajenda inaanzishwa kisiasa ili kujipatia umaarufu wa bure wa kudhani kuwa ndiyo njia ya kuwapeleka ikulu mwaka 2015 jambo ambalo halitawezekana ,maana watanzania hawataweza kukubali’alisema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo Bw.Kajuna aliendelea kusema kuwa Dkt. Slaa amekuwa akimtuhumu Rais Kikwete kuwa ni FREEMASON , “hebu tumuulize huyu mtu amekutana lini na Rais kwenye iman hiyo” na kwamba katika uongozi wake watanzania wameona miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi yetu kwa
ukuaji wa wa pato la Taifa.

No comments:
Post a Comment