Friday, May 17, 2013

SUGU, PROPESA JAY, ROMA MKATOLIKI WAPIGIWA DEBE KUALIKWA KATIKA SHOW YA LADY JAYDEE KUFUATI, BAADA YA MATONYA NA WENGINE KUMTOSA.

 Joseph Mbilinyi aka "Sugu"
 Joseph Haule aka Proffessor Jay"
 R.O.M.A Mkatoliki

 Lady Jay Dee mwenyewe
 K na D wa Maujanja Saplayaz (Kulwa na Dotto)
WAKATI wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wakisubiri kwa hamu kubwa show kali ya Mwanadada Judith Wambura "Lady Jay Dee" ya kuadhimisha kutimiza miaka 13 katika game ya Muziki huo na kutokana na hali ambayo imeendelea kwa baadhi yawasanii mbalimbali waliokuwa wametajwa kushirikiana naye katika show hiyo kujiengua na kutoa sababu kadhaa za kutoshiriki katika Show hiyo (TID, Linah, Barnaba na Matonya).




Wapenzi mbalimbali wa Muziki huo ndani na nje ya nchi wamesikika kutoka katika sehemu mbalimbali haswa katika mitandao ya kijamii (Facebook na Tweeter). 
Wakishauri Msanii huyo kuachana na wasanii hao "njaa kali wenye tamaa za muda mfupi" na kuangalia wasanii wengine wenye kutambua wajibu na kuthamini haki zao na wasanii wenzao badala ya kuishia kutumika kwa maslahi ya watu wachache ambao nyuma na hata mbele ya pazia ni hao hao ambao wamekuwa wakiwakandamiza na kuwanyonya wasanii nchini. 
Aidha kwa kutokujua na wengine kukujua lakini kwa kule kuendekeza/kutanguliza njaa mbele.

Pichani juu ni baadhi ya Wasanii ambao baadhi ya wapezi wa Msanii Lady Jay Dee wameomba wahusishwe katika kutoa burudani katika show hiyo ili kuipa makali zaidi

No comments:

Post a Comment