Rais wa bendi ya Mashujaa Charlz Baba amemvisha pete ya uchumba mchumba wake Rehema Sospet na kuweka wazi kuwa anampango wa kuvunga naye ndoa miezi michache ijayo
Tukio hilo lilifanyika wakati wa uzinduzi wa mauzo ya albamu ya bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa 'Wanakibega' uliofanyika jijini Dar es Salaam mwisho wa wiki
Bendi hiyo ilifanya uzinduzi wa mauzo yake ya albamu yake mpya ya Risasi kidole ambapo onyesho lake lilijaza mashabiki lukuki na kufurahia burudani iliyotolewa na wanamuziki wa bedni hiyo huku wakisindikizwa na FM Academia
No comments:
Post a Comment