Friday, May 10, 2013

HAYA NDO MAJINA 9 YA WATUHUMIWA WALIOLIPUA BOMU KANISANI ARUSHA

Imeripotiwa kuwa jumla ya watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kutuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu lililorushwa katika eneo la Kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi katika parokia teule ya Olasiti siku ya Jumapili, Mei 5, 2013 na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60.

Ripota wa WAPO FM radio alisema majina ya watuhumiwa hao yametajwa kuwa ni:-

  1. Victor Ambrose Calist (20, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
  2. Joseph Yusuph Lomayani (18, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
  3. George Bartholomeo Silayo (26, mkazi wa Olasiti, Arusha)
  4. Mohammed Suleiman Said (38, mkazi wa Ilala, Dar es Salaam, aliyewafuata kwa gari binafsi washukiwa wa ugaidi kutoka kiwanja cha ndege na kuwepeleka hadi hoteli ya Aquiline iliyopo Arusha)
  5. Said Abdallah Said (28, mkazi wa Abu Dhabi, Nchi za Falme za Kiarabu)
  6. Abdelaziz Mubarak (30, Nchi za Falme za Kiarabu)
  7. Jassini Mbaraka (29 mkazi wa Bondeni, Arusha)
  8. Foud Ahmad (28, Nchi za Falme za Kiarabu)
  9. Said Mohsen (Najran, Saudi Arabia)

Hata  hivyo, himaya ya Imarati, Nchi za Falme za Kiarabu (UAE - United Arab Emirates)  inasema maafisa wake wamekanusha kuhusu raia wake watatu kuhusika na mlipuko wa bomu la Olasiti, Arusha.

Abu Dhabi ni mji mkuu wa Imarati (UAE), ambazo zina imirati saba -- Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Fujairah, Ras al Kaimah, Ajman na Umm a Quwain. Nchi jirani na UAE ni Qatar, Saudi Arabia na Oman. 

No comments:

Post a Comment