Thursday, May 9, 2013

Jay-Z kupiga show Diamond Jubilee Dar es Salaam Oct 4 ,2013


image

Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za bara la Africa zilizochaguliwa na rapper Sean Carter aka Jay-Z kwaajili ya kutumbuiza kama sehemu ya ziara yake ya wiki saba ya dunia.
Ziara hiyo ni kwaajili ya kutangaza uelewa kuhusu tatizo la maji duniani. Inatarajiwa kuanza September 9 nchini Poland na kuzunguka mabara ya Ulaya, Africa, Asia na kumalizia Australia.

Barani Africa ataanza na show jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee October 4 kisha Accra, Ghana, Lagos, Nigeria, Luanda, Angola, Cape Town, Durban, na Johannesburg, Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment