Monday, May 13, 2013

REGINALD MENGI ATANGAZA DAU LA MILIONI MOJA KWA MTU ATAYEMTUMIA TWEET NZURI


Upo kwenye Twitter? Kama haupo fanya haraka ujiunge sababu kuna ulaji huko!! Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema kuanzia mwezi huu, atakuwa akitoa shilingi milioni 1 kwa kila tweet itakayomfurashia.

mengi2
Not to fast though…… Sio tweet zile za ‘I’m having fun being single, #TeamSingle, tupa kuleee!

Mengi anataka ulikune jicho lake kwa tweet yenye akili ambayo inaweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupunguza umaskini uliokithiri nchini.
 
“Umaskini umekuwa sugu. Kwa mwaka 1 anzia Mei ntatoa sh 1m kila mwezi kwa tweet nitakayochagua kuwa bora kushinda vita na umaskini,” ametweet leo.
 
Ameongeza kuwa Tweet hiyo iende kwake, yaani mtu akiandika tweet afanye kummention ili aione. 

No comments:

Post a Comment