Mamilioni ya watanzania wanaotumia vinywaji aina ya soda ipo hatarini baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA jumatano linaripoti.
Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa habari Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania-IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya duniani umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji sigara inayosabisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.
Utafiti umeonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji cha soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu.
IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji kuwa makampuni yanayotengeneza soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo.
Utafiti wa IJUTA umeonyesha kuwa utamu wa kupindukia uliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya acid iliyomo ndani ya soda.<--more-->
IJUTA imegundua kuwa kiwango cha acid kilichomo ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa sababu ya kuhofia kuwa watu wakibaini wataacha kutumia kinywaji hicho.
Inaelezwa kuwa madini ya cola yaliyomo yana kilevi cha aina ya kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.
Dr. Mercola wa Marekani amekaririwa na tafiti mbalimbali akieleza kuwa soda ni hatari kwa binadamu sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi.
...Soda yenye chembe za cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya acid na chemicals zinazofichwa vipimo vyake kwa watumiaji.
Wakati utafiti huo ukidhihiriksha hayo, Taasisi ya chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.
SOURCE: MTANZANIA
ISSN : 0856-5678, Na. 7310
Toleo la leo
ukurasa wa 3
ISSN : 0856-5678, Na. 7310
Toleo la leo
ukurasa wa 3
No comments:
Post a Comment