Baadhi ya wabunge na wadau wa elimu wametaka Serikali kutoishia kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, bali iwajibishe Baraza la Mtihani Tanzania (Necta) kwa kufelisha wanafunzi.
Akizungumza kuhusu kauli ya Serikali kufuta matokeo hayo jana, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza alisema taarifa ya tume ingekuwa tofauti na ilivyotolewa ilikuwa isababishe vurugu nchini.
“Kauli hii ya Serikali ndiyo iliyotegemewa na wadau wa elimu, tume wangefanya vinginevyo tunge-riot (fanya vurugu), kwa sababu matokeo yaliyotolewa na Necta siyohalisi. Tume imefanya kazi nzuri na kilio cha wanafunzi kimesikika,” alisema Rweikiza na kuongeza:
“Sasa na hili nalisema bila kificho, Necta lazima wawajibishwe kwa sababu wanafunzi wanne wamejiua kwa matokeo hayo yasiyo halali, kule kwangu (Bukoba Vijijini) wanafunzi wamekata tamaa na wanaolewa. Hiyo yote ni hasara ambayo haina wa kuilipa.”
Aliongeza kuwa nchi nyingi duniani ikiwamo Marekani, mtihani wa mwisho hauchukuliwi kama kigezo kwa sababu inategemea mwanafunzi jinsi alivyoamka siku ya mtihani na kwamba, wanatumia mitihani iliyopita kufanya tathmini yao.
“Necta ni aibu tangu uhuru hawajawahi kufanya mambo ya ajabu kama hivi. Lazima wawajibishwe kwani wanafunzi wamepoteza maisha kwa sababu yao,” alisema.
Mbunge wa Ngara, Deogratias Ntukamazina alisema suala la mfumo wa kuweka viwango haliwezi kuchukuliwa peke yake kwa kusababisha matokeo mabaya.
Ntukamazina ambaye kitaaluma ni mwalimu, alisema suala la kufeli kwa wanafunzi analigawa sehemu mbili; taaluma na maslahi kwa walimu.
Ombi la ziada lazima liangaliwe tofauti na hivi sasa. Serikali inapojaribu kutumia kigezo kimoja cha upangaji matokeo kuwa ndicho kilichosababisha kufeli kwa wanafunzi hao.
“Suala la vitabu, vitendeakazi, mazingira ya kazi, walimu kukata tamaa hatutakiwi kupuuza haya mambo,” alisema Machali.
Alisema suala la maslahi ya walimu lazima Serikali ikae nao hata kama siyo kiwango wanachotaka, lakini iwaongezee kidogo na kwamba, kufutwa kwa matokeo hayo ni jambo zuri lakini siyo mwisho wa tatizo, huku akiongeza kuwa hata alama zikipunguzwa aliyeandika zombi kavaa viatu hatapata kitu.
“Unabadili mfumo wa kupanga matokeo na madaraka, mathalan mwaka jana daraja D ilikuwa alama 35, zamani ilikuwa 21. Hivi hawa wanafunzi umewaandaa kwa sababu walikuwa wameshajipanga kwa 21, huyu wa Zombi hata ungempa mtihani kutwa nzima asingeweza kupata hizo alama,” alisema.
Mbunge huyo alisema suala la elimu halitakiwi kufanyiwa mzaha na Serikali inatakiwa kusema ukweli.
SOURCE:::MWANANCHI:::
Mbunge huyo alisema suala la elimu halitakiwi kufanyiwa mzaha na Serikali inatakiwa kusema ukweli.
SOURCE:::MWANANCHI:::
No comments:
Post a Comment