Gary baada ya kumpiga Amante risasi akijua amemuuwa, alienda kwa Alvira huku akijifanya amelewa. Gary anatamka neno moja ambalo linamshtua Alvira alisema “hakuna kitu kingine kitakacho tuingilia katika maisha yetu”, lakini bado wakiwa wanaongea, bibi wa Amante alimpigia simu akimwambia Amante amepigwa risasi, wanaagana na Gary huku nyuma Alvira akimwaga machozi.
Suzan na MARA na Derick wanafanikiwa kurejea jijini, lakini wanapokea Ujumbe mbaya wa Amante kupigwa risasi. MARA na Suzan wanafika nyumbani. Mama yake Gary anawaonyesha kitu kwa kusonta huku akiwa amejawa na uchu wa kusema kitu, lakini wakati aking’ang’ana kuwaonyesha, Clara anaingia na kuanza kujibizana na vibaya na MARA. MARA namwambia Clara “sikujua kuwa wewe na baba yako Gary mnahusika na kutaka kumuuwa baba yangu, sasa basi wewe na huyo baba yako mtakwenda wote jera.
”.
”.
, Gonga ..
Vilio vya tanda hospitali baada ya Alvira kufika hospitali kumuona mumewe Amante, kiukweli anajuta na kutubu kwa makosa yote aliyomtendea mumewe. Lakini wakati akizungumza maneno hayo, tayari Gary alikuwa kajibanza sehemu akitazama picha yote, kitu kinachomfanya aghadhabike maradufu na kuanza kupiga ngumi ukuta. Jamaa anaamua kurejea nyumbani akiwa ni mwenye hasira, anamkuta Clara na kumweleza kuhusu Alvira, lakini kibaya zaidi Clara anamwambia kuwa “nilikwambia mapema kuwa mama hakupendi” maneno hayo yalimuongezea Gary hasira na kujikuta akimkaba shingo Clara.
Alvira anampigia simu Suzan na kudai kuongea na MARA, alishindwa kuongea bali alimwambia kuwa hali ya baba yake ni mbaya huku akimwaga machozi kama mvua. Gary pia nampigia simu Alvira na kumueleza kuwa yuko nyumbani anakula good time, japokuwa alimtaka arejee nyumbani.
Gary anamkuta Clara akiwa anaelekezwa nje na bibi yake kwa kumnyooshea kidole nje. Gary anang’amua eneo zilipofichwa pesa na kuzifukua pesa hizo zilizokuwa zimechimbiwa na bibi huyo. Tayari Clara amekwisha fanya shoping na kurejea nyumbani, lakini bibi yake anamuomba Clara awasaidie MARA na Suzan, lakini Clara anakataa.
Alvira anarejea nyumbani na kumkuta Gary, Alvira anaulizwa kuwa alikuwa wapi? Lakini Gary anajibu mwenyewe “unatoka kwa Amante!” Alvira kwa jazba anamjibu kuwa “ninae mpenda ni Amante sio wewe”, anakimbia kujifungia ndani huku akiomba msaada kwani Gary tayari alikuwa kashikilia bastora. Gary anabomoa mlango na kumkamata mkono kwanguvu Alvira. Alvira kwa hasira anazidi kumuambia hampendi na anamchukia kwani anampenda Amante.
Alvira akiwa anapiga kelele za kuomba msaada, MARA na Suzan walikuwa wamefika nyumbani kwa Alvira na kusikia kelele, wote wanawafuata huko chumbani. Gary kuona hivyo, anatoa bastora na kumnyoshea Suzan lakini Alvira na MARA wanamzingira Suzan kwa pamoja, lakini Gary bado akiwa na hasira anawauliza “mnafikiri mtakimbia kwenda wapi?” anawanyooshea bastora wote watatu. Wakiwa bado wanajibizana maaskali wanafika, na Avira anawaamuru wamkamate, anakamatwa na kuwekwa ndani.
Huko hospitalini Amante anapata nafuu na kumuulizia Alvira. Clara afanikiwa kufika hospitali kumuona Amante,Je Clara analipi la kufanya ilihali baba yake Gary yuko rumande? Je Gary ataendelea kukaa rumande?
Mwandishi: Vikta Machota (Asili Yetu Tanzania)
To be continue..
No comments:
Post a Comment